Wadada wa Mjini na Tabia ya Kuongeza 000

Wadada wa Mjini na Tabia ya Kuongeza 000

MIE NITOE 10MIL nimpe GF??????????? hahahah dah kwel kuna watu wana akili fupi.. huyo dada nampa BIG UP aendelee kuwanyoosha tu.....
Si wana hela jamani [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna ka ukweli.
Ila kwenye bei za vitu ujue kuna fake na original.
Pia lazima tukubaliane,mnaweza kuwa kwenye circle ya maisha ila mnatofautiana sana kipato.
 
Hahahaaaa yule mmoja aliniambia kodi analipa 600k

Dalali akaniambia wanalipa 250k...

Maisha ni rahisi sana ukiwa huru.
 
Mzigua unashindwa kuafford laki na ishirini,Mimi nakuchuliaga wa gharama kumbe ninnaweza kukuafford na kukupa kila kitu [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kuna ka ukweli.
Ila kwenye bei za vitu ujue kuna fake na original.
Pia lazima tukubaliane,mnaweza kuwa kwenye circle ya maisha ika mnatofautiana sana kipato.
Wakati mwingine duka moja ujue ila anakutajia bei tofauti. Mmoja alienda nunua powder pale vazi nikaipenda nikwambia umenunua sh ngapi akasema kanunua 90k kwenda Vazi naikuta 25k na hamna duka wanauza bongo zaidi ya hapo.
 
Mzigua unashindwa kuafford laki na ishirini,Mimi nakuchuliaga wa gharama kumbe ninnaweza kukuafford na kukupa kila kitu [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
Inategemea nanunua nini mkuu. Siwezi nunua kitu ninachoona napigwa no no no
 
Hii tabia ya kina sisi kuongeza 000 kwenye gharama ya kitu naona imekua fasheni sasa hivi. Mtu kanunua kibanio elfu 10 atakwambia kanunua laki. Kuna mafuta nilimkuta nayo rafiki yangu nikayapenda nikamuuliza umenunua shilingi ngapi akaniambia kanunua 120,000 nikabaki kutoa macho maana hiyo hela sina. Siku Nikapita Kkoo nikakuta same same mafuta yanauzwa 7000 nikajua hapo alitaka kuniringishia anapaka mafuta ya gharama.

Mwingine alinunua gauni 8000 akaulizwa akasema kanunua Mwenge 50000 wakati alikua saluni ikapitishwa 8000 tu akanunua.

Na hii tabia nyingine ya kujiwekea asset mdomoni ili mtu aonekane matawi. Mimi kama sina nasema sina wala sivungi na sioni aibu. Sasa rafiki yangu mmoja kuna siku akawa ananilecture eti nikikutana na mwanaume mwenye hela ili kumlia hela zake nimdangamye nina miradi anisaidie hela.
Kwa mfano akasema nimwambie nina kiwanja bagamoyo anisaidie kujenga nikamwambia mi siwezi uongo ntadakwa tu maana nitajisahau siku.

Kina kaka hawa slay queens wengi mnaowana hata pa kuishi hawanaga wanakaa kwa mashoga ila ukimuona anavyoringa sababu anataka umuone wa gharama umpe pesa nyingi.

Wanaazimaga magari waje nayo kwenye outing ili ukimuona umpe pesa ya mafuta sio nauli ya uber au bajaj.

Kuna kesi niliisikiliza mwanamke alimdanganya mwanaume ana mashamba ya mpunga na amefungua machine ya kusaga na kukoboa kwahiyo amsaidie kiasi kidogo aongeze kununua machine. Yule kaka alimpa 10M baby wake zimsogeze kwenye biashara. Akaja akamwambia gari yake imekwama amsaidie hela aongezee atoe gari kaka akatoa akijua gf wake ana akili ya maisha pale anamsaidia kwa ajili yao. Kumbe alikua hajui zile hela akizitoa wenzie tunaenda zetu brunch Hyatt kuzitumbua pesa za shemeji.

Ila alikua anavyomuona kwanza anajulikana. Anavaa vizuri utasema nani sijui. Nywele za gharama tupu. Duka analoenda ni JM Virgo. Anaishi maisha ya juu kuliko hata uhalisia wake. Ila wanaume wakiona wanapapatika wanampa hela maana wanapigwa fix dada ni self made millionaire wanaingia king kumbe wakitoa anaenda kuvaa apendeze apatikane mwingine ahudumie.

Siku hizi kila mwanamke unaekutana nae atakwambia mwanafunzi mara mfanyabiashara ili tu akuvuteni maana nyie si ndo mnajitia mnapenda hayo kaka zangu kumbe mtu hasomi wala nini anauza k mjini aishi.

NA KINA SISI TUACHE KUONGEZA NAMBA MTU AKITAKA KUKUPA ATAKUPA TU.
Kheeeee makubwa ....hivi kufake maisha ni sifa au ulimbukeni .....unaenda kuazima gari ya mtu hammadi umepata ajari gari iko meng'emeng'e utalipa nini???? Ifike mahala tukubaliane na hali zetu na tujue mpaji ni mungu na fungu lako lipo IPO siku utapata cha msingi kuongeza juhudi na maarifa katika kutafuta riziki yako full stop
 
Wanawake wengi wa Tanzania wameamua rasmi kutumia kiungo chao cha uzazi kupiga pesa,,..hivi huyo jamaa aliyetoa 10m anajielewa kweli??,,au labda na yeye ni millionea!!
Ukiona hivyo ujue milionea ....hawezi toa mil 10 wakati anazo 20
 
Wakati mwingine duka moja ujue ila anakutajia bei tofauti. Mmoja alienda nunua powder pale vazi nikaipenda nikwambia umenunua sh ngapi akasema kanunua 90k kwenda Vazi naikuta 25k na hamna duka wanauza bongo zaidi ya hapo.
Maybe edition tofauti.
Na mara nyingi mtu mdanganyifu anaweza akawa anapenda competition.
Lakini kama kweli mtu kanunua perfume laki tatu,kariakoo ukaikuta ile ile elfu 12000 huenda kweli alinunua bei hiyo alipigwa!
Au kanunua mafuta laki ila matokeo yake bora apake vaseline.
Inatokea sana.
Inshort kuact maisha ni kugumu sana.
 
Kheeeee makubwa ....hivi kufake maisha ni sifa au ulimbukeni .....unaenda kuazima gari ya mtu hammadi umepata ajari gari iko meng'emeng'e utalipa nini???? Ifike mahala tukubaliane na hali zetu na tujue mpaji ni mungu na fungu lako lipo IPO siku utapata cha msingi kuongeza juhudi na maarifa katika kutafuta riziki yako full stop
Zamani ulikuaa mkimyaaaaaa
 
Back
Top Bottom