Wadada wakijiachia wanaangukia kwa wakware, wakibana sana wanaishia kuitwa mashangazi. Sasa wafanyeje?

Wadada wakijiachia wanaangukia kwa wakware, wakibana sana wanaishia kuitwa mashangazi. Sasa wafanyeje?

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Duni hii siyo fair hata kidogo kwa wanawake. Tamaduni hazimpi mwanamke nguvu ya kuamua aolewe lini na aolewe na nani. Hivyo mwanamke hubakia njiapanda.

Mtanziko huu ndiyo umewaingiza wanawake wengi sana kwenye dimbwi la usingo maza.

Katika umri mdogo (early 20s) wanaume wanaowahadaa kuwa wanataka kuwaoa huaminiwa na kupewa tunda, lkn baada ya mimba kunasa wanaume hao huruka kimanga na kuwaacha wadada hao na makovu ya usingo maza.

Wadada wanaowakwepa sana wakware kwa kuwanyima tunda kwa sharti la tendo. (sex) baada ya ndoa, huweza kufika mpk 35 bila kupata ndoa. Wakifikisha umri huo, jamii inaanza kuwananga kwa maneno ya kashfa na kuwaita majina mabaya kama Gumegume, Mshangazi, Nungayembe, n.k.

Ni kutokana na shida hii, ndiyo maana matumizi ya p2 yako juu sana na uchoropoaji mimba imekuwa jambo la kawaida hadi kupelekea matatizo kama kansa ya kizazi na ugumba kuongezeka miongoni mwa wanawake.

Sasa katika kizazi hiki cha nyoka msichana anapaswa afanyeje ili ayafikie matamanio yake ya kujenga familia pasipo kikwazo??

N.B.
1. Ugumba ni ile hali ya kushika ujauzito kwa mbinde sana. Mtoto 1 au 2 mwisho.

2. Utasa ni ile hali ya kutokuwa na uwezo wa kushika mimba kabisa.
 
Back
Top Bottom