Wadada wanapendelea zaidi marashi ya kiume kwa sababu huwa yananukia vizuri

Wadada wanapendelea zaidi marashi ya kiume kwa sababu huwa yananukia vizuri

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Katika kukutana na kuongea kwangu na baadhi ya wadada, iwe hapa bongo na hata ughaibuni, nimeshasikia wakisema kuwa wao wanapendelea zaidi marashi [pafyumu, deodorant, na body sprays] ya kiume kwa sababu huwa yananukia vizuri.

Niliwahi kuwa na mfanyakazi mwenzangu mmoja hivi aliyewahi kunambia kuwa yeye hutumia viondoa harufu [deodorant] vya kiume.

Nilimshangaa kidogo pindi aliponambia hivyo. Niliona ni kitu cha ajabu kwa sababu sipati picha njemba kutumia marashi ya kike.

Baadaye tena nikakutana na mdada mwingine naye akanambia kwamba yeye anapenda kutumia 'pafyumu' za kiume. Nikaguna kidogo...halafu nikamkumbuka yule mfanyakazi mwenzangu.

Basi, nikadhani labda ni hao wawili tu. Siku moja niko nyumbani chumbani nasikia mlango unagongwa....kuuliza nani huyo? Nikasikia sauti ya dada binamu...eti anaomba kujipulizia unyunyu wangu wa Bottega Veneta!

Kumwuliza kwa nini unataka unyunyu wangu ambao ni wa kiume? Nikapata jibu lilelile...eti unanukia vizuri! Khaaa!

Sasa nikabaki najiuliza....hivi ni kweli marashi ya kiume wadada wanayependa kihivyo?

Ningependa kusikia toka kwa wadada wa JF pia kama haya niliyoyasikia ni ya kweli.

Karibuni.....
 
wanaopaka hizo za kiume huwa wanamunzi mwenza pindi awapo mbali,. i mean endapo boy wad alikuwa anapaka NIVEA basi akiwa mbal nae anaipaka il afeel kuwa bado yupo, so ukiona mpenziO anapaka perfum ambayo hupak wew ujue mpo wa2.
 
wanaopaka hizo za kiume huwa wanamunzi mwenza pindi awapo mbali,. i mean endapo boy wad alikuwa anapaka NIVEA basi akiwa mbal nae anaipaka il afeel kuwa bado yupo, so ukiona mpenziO anapaka perfum ambayo hupak wew ujue mpo wa2.

Ayaaaa weee, ndo hivyo kumbe?
 
mkuu umetisha sana kwa kuweka Bottega nyumbani

mengine tuwaachie wakinadada na wanaume wa Dar watakua wanaelewa sana hizi mambo..
 
mkuu umetisha sana kwa kuweka Bottega nyumbani!

Bottega ziko poa sana.

upload_2016-4-5_11-37-31.png
 
Hata mimi nazipenda sana tu,marashi mengi ya kiume yametulia Yako ndani kwa ndani ,hayakeri in short Yako cool Sana ,mara nyingi yakike harufu Kali sana kwa upande Wangu yananiumiza sana kichwa.
 
Mhhhhhh weee utakua umezoooeee za elfu tanoo 5000 Acha kutupangaaa
 
View attachment 335052
Nilijua uliwahi kuitumia, Nasikia ni nzuri sana mimi binafsi sijawahi kuitumia pia bei ni Tsh.@20,000/= kuna jamaa aliniambiaga dukani sasa moja kwa moja nkajua pafyum nzuri ni from 35,000 kwenda juu lkn baadhi wanasema ni pafyum nzuri kwa wanaume pia

Duh!

Ndo kwanza naiona leo hiyo.
 
Back
Top Bottom