Wadada why this

SMART1

Senior Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
133
Reaction score
48
Hivi kwa ninyi madada, mawifi, mama wakwe.....
Hivi ni kwanini mwanamke mwenzenu anapochelewa kupata mtoto akiwa ndani ya ndoa huwa mnapenda kuwasimanga. Mara mjaza choo, anakula vya mwanao/kaka ako bure.
Hamjui alie kuwa wewe ndio amemnyima yeye. Au bado anasubiri majira ya Bwana!
please muwaombee badala ya kuwadharau!!
 
Unazungumzia wanawake wa uswazi naona....
 
SMART1,

Hivi kuna watu (mwanamume na mwanamke) wanaooana bila kutarajia kupata mtoto?
 
Wala sio uswazi tu, hata wale waliostaarabika wana tabia hiyo.


Hapa Laura nadhani anazungumzia hata wale ambao sio wa uswazi, walioenda shule! ila hii inanisikitisha sana. Nashindwa sometimes kuwaelewa hawa wadada!
 
SMART1,

Hivi kuna watu (mwanamume na mwanamke) wanaooana bila kutarajia kupata mtoto?

Hilo unalozungumza ni kweli, kuwa ndoa nyingi zinategemea kuwa na watoto
Basi tujiulize ni nani anaetoa baraka ya watoto, Only God... so we have to walk on the God's will.
 
ni kutokuwa na uelewa siku hizi rate ya wanaume na wanawake kutokuzaa ni kama sawa tu.
 
Inasikitihsa sana. Ivi sara na Ibrahimu nao walisemwaga?
 
Sio tabia nzuri kwakweli na kuna baadhi ya wanaume nao huchangia katika hili. Yaani kutwa kucha wao ni kulalamika tu kusikokua na mwisho hadi anawapa kiburi hata hao ndugu zake!
 
Jamani ni kweli inasikitisha sana utadhani hao wanawake wanaosemaga wenzao hovyo walipata watoto kwa kutaka wao, kumbe ni Mungu aliamua kukupa tu mtoto, na hata hukujua utazaa dume au jike, ni Mungu tu alikupa kwa neema, na akiamua kuwachukua huwezi hata kupingana naye. Tuwe na huruma jamani si kuropoka tuuuuuuuuuu, Mungu atakupiga kibao bure ushangae!!!!
 
Sio tabia nzuri kwakweli na kuna baadhi ya wanaume nao huchangia katika hili. Yaani kutwa kucha wao ni kulalamika tu kusikokua na mwisho hadi anawapa kiburi hata hao ndugu zake!

Unajua kulalama kwa wanaume kunaletwa na mama yake mzazi, dada zake na mashangazi zake.... so it begins from you women
 
Unajua kulalama kwa wanaume kunaletwa na mama yake mzazi, dada zake na mashangazi zake.... so it begins from you women
Ni kweli kabisa wala sikubishii mkuu. Na itakuwa vizuri iwapo masuala yahusuyo kuzaa wangeachiwa wanandoa wenyewe na sio kupangiwa na watu wengine kama hao. Inauma sana kusimangwa na binadam wenzeko ilhali wote twategemea majaaliwa ya mwenyezi Mungu. Natamani wote wabadilike na kuweza kuifeel hiyo hali ya wanaosimangwa labda watakuwa na huruma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…