Wadaiwa sugu vyuo vikuu kutopewa hati za kusafiria nje ya nchi

Wadaiwa sugu vyuo vikuu kutopewa hati za kusafiria nje ya nchi

Curious Naturally

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2013
Posts
528
Reaction score
523
Wadau, nimesikia kuwa wadaiwa sugu vyuo vikuu kutopewa hati za kusafiria nje ya nchi, kutoka "power breakfast" clouds fm, kwenye uchambuzi wa magazeti

Kiukweli binafsi nimeshtuka sana. Sidhani kama huu utakuwa ni uamuzi sahihi. Nchi hii ya ajabu kweli

Huo unaona sio uamuzi sahihi ila kutokulipa ndio uamuzi sahihi? wanasema hata kama huna kazi nenda kareport wajue uko wapi na unafanya nini.
 
wewe ndo utakuwa mtu wa maajabu, kama hujalipa wewe ulitegemea alipe nani? watoto wa maskini wa kizazi kijacho watalipiwa na nani? nina mashaka wewe hujalipa ni mdaiwa sugu na sasa unaomba passport kwenda 'ZARI ALL WHITE PARTY' ya huko uganda baada ya kuteketeza million 3 pale mliman juzi, hebu mara hii kalipe hizo za party utapata mbelen
 
Hizi ndizo tabia zinazoturudisha nyuma kimaendeleo, yaani mtu unashimdwa kulipa mkopo ambao unadaiwa halafu unawaza kwenda nje ya nchi. Naona uamuzi wa serikali upo sahihi kabisa, tena ikibidi wafilisiwe kabisa.
 
wazo langu kwa serikali wadaiwa wengi wapo kwenye halmashauri zetu,wafanye msako wa hawa wadaiwa huko watawapata wengi,wakisubiri wadaiwa waende wenyewe itakua historia kulipa,wawape jukumu hili wakurugenzi wote nchini kusubmit watumishi wote wanaodaiwa na bodi,wahusika chukueni hiyo mbinu,ikiwezekana hata wakuu wa shule waratibu elimu kata wakuu qa idara etc wahusishwe katika kutoa taarifa za hawa watu
 
Wadau, nimesikia kuwa wadaiwa sugu vyuo vikuu kutopewa hati za kusafiria nje ya nchi, kutoka "power breakfast" clouds fm, kwenye uchambuzi wa magazeti

Kiukweli binafsi nimeshtuka sana. Sidhani kama huu utakuwa ni uamuzi sahihi. Nchi hii ya ajabu kweli

Hivi kwanza wadaiwa sugu anaanzia mwaka gani hadi waliomaliza mwaka gani au hata waliomaliza mwaka jana,juzi na 2012 nao ni wadaiwa sugu?
 
walipe kwanza wabunge na mawaziri waliotangulia kusoma enzi hizo tena kwa gharama kuubwa na anasa,
hela ya mkopo yenyewe nilisotea bodi ya mkopo oale ofisini kwao miez 3 hata haina faida ya kuillipa....
hili swala la kutulazimisha vijana tulipe na wao wazee kujitow litaleta nalo mgomo siku moja, just matter of time.. ...
mshahara kiduchu, makato lundo, bado wakomalie na huu upuuzi.....
mnaotetea ni wale mliosomeshwa bure kwa gharama za juu mkienda cafeteria mnachamvua nyama za kuku.....
 
wazo langu kwa serikali wadaiwa wengi wapo kwenye halmashauri zetu,wafanye msako wa hawa wadaiwa huko watawapata wengi,wakisubiri wadaiwa waende wenyewe itakua historia kulipa,wawape jukumu hili wakurugenzi wote nchini kusubmit watumishi wote wanaodaiwa na bodi,wahusika chukueni hiyo mbinu,ikiwezekana hata wakuu wa shule waratibu elimu kata wakuu qa idara etc wahusishwe katika kutoa taarifa za hawa watu

wewe umewalenga walimu moja kwa moja... (mambo ya wakuu wa shule..waratibu elimu)...

HUYO MKURUGENZI MWENYEWE UNAWEZA UKAKUTA NI LOAN DEFAULTER na hajajipeleka... na vipi kuhusu kada nyingine!? hao hawapaswi kufuatiliwa kwa ukaribu....
HAPO SUALA NI KUWEKA MFUMO WA UFUATILIAJI UTAKAOWANG'AMUA WALIOFAIDIKA NA MKOPO WA ELIMU YA JUU... MBONA MFUMO WA KUJUA WAAJIRIWA WA SERIKALI (KIMISHAHARA) UPO.
 
Walimu ndo no1 maana ni wengi na 99% wanao mkopo
 
Walimu ndo no1 maana ni wengi na 99% wanao mkopo

je unatambua ya kuwa walimu wenye cheti na diploma tanzania ni wengi kuliko hao wenye degree(ambao wengi wao walioata mkopo).... sasa inakuwaje unasema walimu wachache miongoni mwa kundi la walimu wengi wasiosomeshwa kwa mkopo kuwa ndio asilimia 99!!!??...THINK BIG..
TUKIRUDI KWENYE MADA YETU..SERIKALI INAPASWA KUWAFUATILIA WADAIWA WOTE BILA KUJALI WAPO KADA GANI YA AJIRA...
 
safi sana serikari kwa uamuz huo coz hata wanafunz wengne wanahtaj kusom kupitia huo mkopo.
 
Hilo sio jipya katika tangazo lao rasmi mwaka 2012 heslb walisema wadaiwa sugu wanapigwa faini riba ya asilimia 10 toka 5 kwa kuchelewa na pia watawapeleka polisi. Japo niliwaandikia nikawapa details zangu walinijibu wakishkuru tu na mwaka wa nne sasa hawajaanza kukata mkopo wao ambao hata sijui ni sh ngapi. wafanyakazi wengine wameshaanza kukatwa. Jamaa wamekopa benki bodiilivyokata mtu anabaki 50,000 tu hahaha
 
Back
Top Bottom