Wadaiwa wa bodi ya mikopo jioneeni

Wadaiwa wa bodi ya mikopo jioneeni

mmteule

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
5,883
Reaction score
14,600
Habari zenu wanajamvi
Najua baadhi yetu humu jamvini wapo wadaiwa wa Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu.

Napenda kuwatahadharisha kwamba Bodi ya mikopo imeingia ubia na makampuni ya binafsi kwa ajili ya kudai mikopo kwa wadaiwa wake.

Sipendi kuyataja makampuni hayo hapa jamvini, lakini kinachofanyika kwa sasa siyo haki tena kwa Wadaiwa wa mikopo hii. Nipende kuweka wazi kwamba sheria na kanuni za Utumishi wa Umma zinamtaka mwajiri ndiye awasilishe majina ya waajiriwa wake kwenye bodi ya mikopo mara tu anapoajiri mtumishi mpya, akishindwa kufanya hivyo basi yeye ndiye mwenye makosa na anatakiwa apigwe faini kwa kushindwa kufanya hivyo.

Lakini badala yake imekuwa tofauti na kanuni za Utumishi zinavyoelekeza, Makampuni ya kudai mikopo yanapita nchi nzima kwenye Taasisi za serikali kukusanya majina ya watumishi.

waliofaidika na mkopo wa elimu ya juu. Baadae wanapeleka majina hayo bodi ya mikopo, wanachokifanya bodi ya mikopo ni kutoza faini ya asilimia kumi (10%) kwa kila mdaiwa ili kuilipa kampuni ya iliyopewa zabuni. Faini ya 10% inakokotolewa kutoka kwenye principal loan ( Jumla ya mkopo wote) wa mkopaji/mfaidikaji wa mkopo wa Elimu ya juu.

Nipende kuweka wazi kwamba Bodi ya Mikopo mnachofanya ni kinyume na kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma. Anayetakiwa kutozwa faini ni mwajiri, ama kwa vile nyinyi ndio mnadhamana ya kukusanya madeni ndio mnatakiwa kuwalipa wazabuni mliowapa kazi ya kuwasidia kazi ya kukusanya madeni.

Mbaya zaidi baadhi ya wadaiwa wanapofika bodi ya mikopo sikuhizi kuomba kupatiwa kiasi wanachodaiwa ili wafanye utaratibu wa kurejesha hawapewi ushirikiano wowote na watumishi wa bodi ili kutoa mwanya kwa makampuni yao ya udalali kupata 10%.

Kwa taarifa hii naomba wadaiwa wote muwe macho msikubali kuvurutwa na kuibiwa 10% ya mkopo wako ili kulipa makampuni ya wajanja yaliyoiweka bodi ya mikopo mfukoni ili kujinufaisha.
My take, ilichotakakiwa kufanya bodi ya mikopo ni kuwataarifu/ kuwakumbusha waajiri wote nchini kuwasilisha haraka majina ya wafaidika wa mikopo ya elimu ya juu ili waanze kuwakata. Na mwajiri asiyetekeleza angepigwa faini kama kanuni zinavyoelekeza.

Ama bodi ya mikopo kwa kutumia watumishi wake ilitakiwa watume waajiriwa wao Kwa waajiri wote nchini kukusanya taarifa za wafaidika wa mikopo ya elimu ya juu na kuzifanyia kazi.

Lakini kilichofanyika kutafuta makampuni binafsi na kuyaajiri kwa fedha za walalahoi/wakopaji kutozwa 10% ya mkopo wao ni wizi wa mchana. Nasikitika kusema kwamba bodi ya mikopo hamjatenda haki.

Kwa mantiki hii naomba wakopaji wote kulaani kitendo hiki. Mfano. Mhitimu wa udaktari pale IMTU anayedaiwa mil. 32 za masomo yake atapigwa faini ya 10% shilingi 3,200,000/ ambazo zinalipwa kwa makampuni ya wajanja kisa tu kampuni hiyo imeenda kwa mwajiri kuchukua jina na kulipeleka bodi ya mikopo.

Haivumiliki nasema. Wakati naandika hivi kuna mamia ya watumishi wanakatwa upuuuzi huuu. MKO WAPI TUCTA, WAPI WIZARA YA KAZI, WAPI KATIBA NA SHERIA, WAPI UTUMISHI?
Tuamke sasa
 
Asante kwa taarifa yako nzuri.
Swali kwa bodi: Ambaye, hajajiliwa popote na hana kazi wala kipato atalipaje deni?
 
Habari zenu wanajamvi…
Najua baadhi yetu humu jamvini wapo wadaiwa wa Bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu. Napenda kuwatahadharisha kwamba Bodi ya mikopo imeingia ubia na makampuni ya binafsi kwa ajili ya kudai mikopo kwa wadaiwa wake.
Sipendi kuyataja makampuni hayo hapa jamvini, lakini kinachofanyika kwa sasa siyo haki tena kwa Wadaiwa wa mikopo hii. Nipende kuweka wazi kwamba sheria na kanuni za Utumishi wa Umma zinamtaka mwajiri ndiye awasilishe majina ya waajiriwa wake kwenye bodi ya mikopo mara tu anapoajiri mtumishi mpya, akishindwa kufanya hivyo basi yeye ndiye mwenye makosa na anatakiwa apigwe faini kwa kushindwa kufanya hivyo.
Lakini badala yake imekuwa tofauti na kanuni za Utumishi zinavyoelekeza, Makampuni ya kudai mikopo yanapita nchi nzima kwenye Taasisi za serikali kukusanya majina ya watumishi waliofaidika na mkopo wa elimu ya juu. Baadae wanapeleka majina hayo bodi ya mikopo, wanachokifanya bodi ya mikopo ni kutoza faini ya asilimia kumi (10%) kwa kila mdaiwa ili kuilipa kampuni ya iliyopewa zabuni. Faini ya 10% inakokotolewa kutoka kwenye principal loan ( Jumla ya mkopo wote) wa mkopaji/mfaidikaji wa mkopo wa Elimu ya juu.
Nipende kuweka wazi kwamba Bodi ya Mikopo mnachofanya ni kinyume na kanuni na taratibu za Utumishi wa Umma. Anayetakiwa kutozwa faini ni mwajiri, ama kwa vile nyinyi ndio mnadhamana ya kukusanya madeni ndio mnatakiwa kuwalipa wazabuni mliowapa kazi ya kuwasidia kazi ya kukusanya madeni.
Mbaya zaidi baadhi ya wadaiwa wanapofika bodi ya mikopo sikuhizi kuomba kupatiwa kiasi wanachodaiwa ili wafanye utaratibu wa kurejesha hawapewi ushirikiano wowote na watumishi wa bodi ili kutoa mwanya kwa makampuni yao ya udalali kupata 10%.
Kwa taarifa hii naomba wadaiwa wote muwe macho msikubali kuvurutwa na kuibiwa 10% ya mkopo wako ili kulipa makampuni ya wajanja yaliyoiweka bodi ya mikopo mfukoni ili kujinufaisha.
My take, ilichotakakiwa kufanya bodi ya mikopo ni kuwataarifu/ kuwakumbusha waajiri wote nchini kuwasilisha haraka majina ya wafaidika wa mikopo ya elimu ya juu ili waanze kuwakata. Na mwajiri asiyetekeleza angepigwa faini kama kanuni zinavyoelekeza.
Ama bodi ya mikopo kwa kutumia watumishi wake ilitakiwa watume waajiriwa wao Kwa waajiri wote nchini kukusanya taarifa za wafaidika wa mikopo ya elimu ya juu na kuzifanyia kazi.
Lakini kilichofanyika kutafuta makampuni binafsi na kuyaajiri kwa fedha za walalahoi/wakopaji kutozwa 10% ya mkopo wao ni wizi wa mchana. Nasikitika kusema kwamba bodi ya mikopo hamjatenda haki.
Kwa mantiki hii naomba wakopaji wote kulaani kitendo hiki. Mfano. Mhitimu wa udaktari pale IMTU anayedaiwa mil. 32 za masomo yake atapigwa faini ya 10% shilingi 3,200,000/ ambazo zinalipwa kwa makampuni ya wajanja kisa tu kampuni hiyo imeenda kwa mwajiri kuchukua jina na kulipeleka bodi ya mikopo. Haivumiliki nasema. Wakati naandika hivi kuna mamia ya watumishi wanakatwa upuuuzi huuu. MKO WAPI TUCTA, WAPI WIZARA YA KAZI, WAPI KATIBA NA SHERIA, WAPI UTUMISHI?
Tuamke sasa

Dawa ya deni kulipa, ukilipa hayo yote hayatakukumba
 
Dawa ya deni kulipa, ukilipa hayo yote hayatakukumba

Wazano records lakini maana wao wanachofanya ni kupiga ramli hasa wale wa zamani mtu udaiwi lakini kama ulisoma enzi hizo unao, ngoja nitayarishe mkuki wangu hapa
 
Kwakuwa limkopo lenyewe nililipata kwa taabu sana hivyo deni Lao nao watalipata kwa taaabu vilevile,zam kwa zam malipo ni hapahapa.
 
Kwa kumbukumbu yangu nilipoe nda heslb 3 yrs ago kuchukua statement ya deni langu... ninayo hadi leo.

Ukiprintiwa statement inaonyesha deni lako unalo takiwa ulipe effectivelly ukimaliza chuo, na wameonursha sehemu ya fine kama ukichelewa kulipa kuna sehenu ya fine wameweka 10% hiyo utafanyiwa mahesabu ukienda kujaza ile fomu ya repayment ndo wanaangalia umechrlewa muda gani una pigwa fine.

Ila nilikuwa sijui kumbe ile kitu hatulipi sisi ni mwajori wetu eeh.. hahaha hv mhindi wangu atakubali aanze gu kunilipia deni langu.
 
Back
Top Bottom