Wadau hawa Wakubwa wa elimu wamepotelea wapi ?

Wadau hawa Wakubwa wa elimu wamepotelea wapi ?

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,522
Reaction score
37,398

Wadau hawa Wakubwa wa elimu wamepotelea wapi?​

By Hata Mimi JF member​

Salaam alaikum,

Zamani kabla ya 2010 kurudi nyuma huko tulizoea kuona vitabu vya namna mbalimbali kwa maudhui moja. Namaanisha somo husika kwa darasa fulani linakuwa na matoleo kibao ya vitabu (waandishi na wachapaji)

Hii ilikuwa inasaidia wadau kuchagua vitabu wanavyoona wao vitawasaidia na nakumbuka ikawa inaleta ushindani fulani kwenye maendeleo ya elimu yetu. Kwa vyovyote vile mabadiliko tuliyopiga katika elimu yetu inaonesha wale waandaaji wa vitabu vile wamesaidia sana mpaka kufika hapa tulipo

Sasa cha ajabu kumekuja utaratibu huu wa kwamba vitabu vyote vinaandaliwa (uandishi na uchapaji) na Taasisi ya Elimu Tanzania ndo basi tena sijawahi kuona tena vikitolewa vitabu tofauti na hivyo vya Taasisi ya Elimu Tanzania

Mashaka yangu (au niseme swali langu) ni kama hawa watu wamezuiwa kuandaa vitabu hivyo au nini? Maana kwa zama tulizonazo sasahivi naona kama wangeendelea ingeleta tija zaidi lakini siyo hii ya kila kitu kutolewa na Taasisi ya Elimu.

Binafsi naona hata mvuto ule umepotea sasahivi siyo kama enzi zile unakuta mtoto asipoelewa kitabu hiki anakwenda kuelewa kwenye kitabu kile kingine. Kwa mfano nakumbuka enzi tunasoma ilikuwa mtu mwenye vitabu vya Oxford ndiye mjanja na hata bei zake zilikuwa juu kidogo kulinganisha na wengine. Kwa wale wa Lugha nakumbuka vitabu vya English vya kampuni moja kutoka Kenya vilikuwa vinauza sana. Sasa hivi hawa Tanzania Institute of Education watakavyoandika ndo hivyohivyo mtoto itabidi akomae anataka, hataki ni wao wameshaandika.

Nitataja mifano ya wachapishaji wa zamani (2008 kurudi nyuma) kabla kuja hii Taasisi ya Elimu Tanzania
Mture Educational Publishers
Educational Books Publishers
Oxford University Press (T) LTD
Macmillan (Aidan Publishers)
Ben and Company LTD
Wizara ya Elimu na Utamaduni
 

Wadau hawa Wakubwa wa elimu wamepotelea wapi?​


30 May 2026

Mture Educational Publishers Limited katika mgogoro wa kimkataba na National Housing Building Research Agency Tanzania

View: https://m.youtube.com/watch?v=MQplIdC7hJE
Wakili Peter Madeleka atembelewa na Bi. Riet Elibariki Moshi mmoja wa wakurugenzi wa Mture Educational Publishers Limited kampuni ya kiTanzania iliyoanzishwa mwaka 1986 na kusajiliwa BRELA mwaka 1997 ikiwa imejikita katika uchapishaji vitabu na vifaa vya elimu na kuvisambaza kwenye mashuleni baada ya kupewa kazi na wizara ya elimu na ufundi Tanzania. Kabla ya 2015 serikali haikuwa inachapisha vitabu bali imejikita ktk kutunga sera na mitaala hivyo kuwagawia kazi kampuni mbalimbali

Mwaka 1997 kampuni wa Mture Educational Publishers Limited baada ya kusajiliwa ilienedesha shughuli zake kutoka jengo lililopo Mwenge jijini Dar es Salaam la Building Research Unit inayojulikana kama National Housing Building Research Agency Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi chini ya chuo kikuu cha Ardhi kwa mkataba maalum 1999 ...
 
nyambari nyangwine wapi sasa ndg mwanazengo alisababisha nionekane mtoto wa mwalimu kumbe apeche alolo...!!
 

Wadau hawa Wakubwa wa elimu wamepotelea wapi?​

By Hata Mimi JF member​

Salaam alaikum,

Zamani kabla ya 2010 kurudi nyuma huko tulizoea kuona vitabu vya namna mbalimbali kwa maudhui moja. Namaanisha somo husika kwa darasa fulani linakuwa na matoleo kibao ya vitabu (waandishi na wachapaji)

Hii ilikuwa inasaidia wadau kuchagua vitabu wanavyoona wao vitawasaidia na nakumbuka ikawa inaleta ushindani fulani kwenye maendeleo ya elimu yetu. Kwa vyovyote vile mabadiliko tuliyopiga katika elimu yetu inaonesha wale waandaaji wa vitabu vile wamesaidia sana mpaka kufika hapa tulipo

Sasa cha ajabu kumekuja utaratibu huu wa kwamba vitabu vyote vinaandaliwa (uandishi na uchapaji) na Taasisi ya Elimu Tanzania ndo basi tena sijawahi kuona tena vikitolewa vitabu tofauti na hivyo vya Taasisi ya Elimu Tanzania

Mashaka yangu (au niseme swali langu) ni kama hawa watu wamezuiwa kuandaa vitabu hivyo au nini? Maana kwa zama tulizonazo sasahivi naona kama wangeendelea ingeleta tija zaidi lakini siyo hii ya kila kitu kutolewa na Taasisi ya Elimu.

Binafsi naona hata mvuto ule umepotea sasahivi siyo kama enzi zile unakuta mtoto asipoelewa kitabu hiki anakwenda kuelewa kwenye kitabu kile kingine. Kwa mfano nakumbuka enzi tunasoma ilikuwa mtu mwenye vitabu vya Oxford ndiye mjanja na hata bei zake zilikuwa juu kidogo kulinganisha na wengine. Kwa wale wa Lugha nakumbuka vitabu vya English vya kampuni moja kutoka Kenya vilikuwa vinauza sana. Sasa hivi hawa Tanzania Institute of Education watakavyoandika ndo hivyohivyo mtoto itabidi akomae anataka, hataki ni wao wameshaandika.

Nitataja mifano ya wachapishaji wa zamani (2008 kurudi nyuma) kabla kuja hii Taasisi ya Elimu Tanzania
Mture Educational Publishers
Educational Books Publishers
Oxford University Press (T) LTD
Macmillan (Aidan Publishers)
Ben and Company LTD
Wizara ya Elimu na Utamaduni
Walishatangulia mbele ya haki kina warumi
 
Ngumu sana waswahili kuheshimu mikataba, kampuni hii Mture ina mguso kimataifa kwa kufanya biashara ya uchapaji kimataifa.

Je wasomi ktk ngazi za maamuzi walikariri hadi kupata vyeti bila kuelimika hivyo kukosa uwezo kufanya maamuzi sahihi barani afrika ?

TOKA MAKTABA :
Kigali, Rwanda

EA Debate Quality Tertiary Education took place in Kigali in July.

View: https://m.youtube.com/watch?v=Rr0QGRRmqgU
It was hosted by the Sustainable Development Goals Centre for Africa and the objective was to create a coalition of African intellectuals to address themes relevant to SDG implementation in tertiary education and research.
 
Back
Top Bottom