najua we ni msomi lakini siku zote uchangiaji wako umekaa kishabaki na kuponda baadhi ya vyuo na kozi.
kama ungekuwa msomi wa kweli ungekuwa unatoa soln kwa matatizo husika mwisho wa siku elimu yako inaonekana msaada kwako binafsi na kwa taifa kwa ujumla.
kumbuka nchi kubwa kama tz yenye watu zaidi ya milion 43 inatakiwa iwe na vyuo vikuu vingi,sio rahisi wanafunzi wote kusoma udsm au sua.
binafsi nimesoma secondari ya kata o level, lakini Alevel nimesoma special school na university nimebahatika kusoma chuo kikuu kikongwe kabisa apa afrika mashariki lakini kamwe simwezi kumzalau mtu aliyesoma udom au vyuo vingine unavyoviita vya kata.
mzee mpiga msuli we ni msomi kuwa sehemu ya mabadiliko ya kile unachokiitaji kuliko kutumia mda mwingi kuonyesha umahiri wa kozi uliyosoma au shule/ chuo ulichosoma.