Sikio ni moja kati ya milango mitano ya fahamu katika mwili wa binadamu.
Kazi yake ni kunasa mawimbi ya sauti.
Mbu akiwa mbali na sikio, mawimbi ya sauti yake hayawezi kulifikia sikio, na hivyo huwezi kusikia sauti yake ingawa sauti yake ingalipo. Akirukaruka eneo la miguuni, huwezi kusikia sauti yake ingawa anatoa. Lakini mbu huyohuyo akiruka karibu na sikio, utaisikia sauti yake.
Hivyo sio sahihi kwamba mbu anatafuta sikio tu, bali huzunguka mwili mzima na akifika sehemu ya sikio mawimbi ya sauti hunaswa na kusikika.