Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Job Ndugai ni Spika wa Bunge la Tanzania , huu ni wadhifa mkubwa mno, mtu mwenye cheo hiki anastahili kupendwa na kuheshimiwa na kila mtu katika nchi hii , Huyu ni kiongozi wa Mhimili muhimu mno wa Bunge.
Lakini cha kushangaza ni hiki , Baada ya uongozi wa Simba kumteua Ndugai kuwa Mgeni Rasmi kwenye Tamasha muhimu la Simba day watu wengi wameshang'aa na kupigwa butwaa , wengi wanapinga Ndugai kupewa heshima hiyo huku wakidai hastahili , si mwanamichezo na wala hana mvuto kwenye siasa za nchi hii , kimsingi kumteua huyu kuwa Mgeni rasmi kumeleta kama nuksi kwenye Tamasha hilo , Ni kama kuweka nazi kwenye supu .
Wako waliojiapiza kwamba Muda ambao Ndugai ataingia uwanjani wao watajiondokea zao , hata kama wamelipa pesa zao.
Kwa mnajua mambo ya namna hii, Jambo hili ni ishara ya kitu gani?