Wadau mliofanikiwa kwenye Forex, kwa mpango wangu huu nami nitafanikiwa ama nitaangukia pua?

Too early to say something on your dream either way is not Easy. Wishing you nice dream
 
[emoji23][emoji1787] forex ni very simple njia ya kuish hasa kibongo huku ukiwa unafanya michongo mingine.
Binafs forex kwangu ni investment hata mshahara ukichelewa huwa nachukua hela huku natumia mshahara ukirud nairudisha[emoji23].

Kwang mm nimetumia mwaka mmoja kujua nn forex inataka na nn haitak.

Hizo kelele zooote watu wanazo piga kwenye mitandao haziwez kukupa chochote,
Jiulize swali.kama mtu anatengeneza 1000usd kwa siku.kwann anakomaa akufundishe wewe[emoji1787].

Kiufupi huo mpango unao upanga unaweza uka kupa result au ukaangukia pua vzr tu

Ila kama unataka kuish na forex kwa raha fanya haya ata usihangaike kupoteza muda.

1. Analysys
2. Target yako ni nn
3.entry
4.a perfect area to put ua stoploss
5.risk management narudia tena risk management narudia tena risk management[emoji23].

Utafanya huo mpango wako miaka yote unayojua ww usipo iva hii misingi mitano.

Tutakuona ukirud tena jamii forum ukiiponda forex ni scam[emoji1787],
Huku wengine wakikushangaa wanaona wanalipa kodi wanakula kwaajil ya forex
 
Na mwaka mzima unasotea kudouble account ni bora ukatafuta robot moja ukaliset likupe 10% ya investiment yako kwa mwezi ukaendelea kufanya mambo mengine kuliko kuteseka bure.
 
Forex ni kama betting...Tena bora betting
1.Forex ni Vs wazungu na mbaenk
Betting ni Vs Wahindi na betting companies

2.betting unakuwa unazijua tim
Forex hujui market(unstability)

3.Betting rahisi kumasta
Forex ngumu kumasta

4.Betting hawapangi matokea lakini wanalimit odds
Forex wanacontrol matokeo

5.Betting unaweza kuulamba lakini forex you are guaranteed to loose
 
Moja Kati ya reply bora kabisa kuwahi kutokea jf [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mzee..Kama unapesa ya kupoteza ingia huko..nilichogundua huna uvumilivu wa kutatua changamoto ndogondogo..Kama mpaka kazi zako mwenyewe zilikushinda tutafanikiwa kwenye lipi!?

Pia unaharaka ya mafanikio kwa kujenga msingi hewa wa hayo mafanikio..
 
Sjui Kwa nn watu hawaelewi hili , in short Forex ni kubahatisha ..... Kuna watu wanacontrol soko , hakuna formula maalum ...... Japo kuna watu wenye nyota ya kubahatisha lakn still ni risk , 95% ya watu wanaloose af useme mi normal kama business zingine , hyo ni bonanza iliyochangamka
 
Na ipo complicated makusudi ili kuwavuta maboya...utaambiwa unaliwa kwasababu ya strategy mbovu au psychology au hufatilii news nk. nk. unakuta unajipa moyo unaendelea kutrade kuwapa hela wazungu.
Utaambiwa forex ni betting kwa wale wasioijua vizuri
Lakini utakuta wanaoijua vizuri hawatrade ila wanauza forex lessons au signals
 
ukifuata hayo uliyoyaandika kwenye fx utatoboa mkuu otherwise utakuwa unafanya gambling na pesa ako
 
Bonanza iliyochangamka😂😂😂
 
Forex sio rahisi kama wengi tulivyoaminishwa!
 
Usisahau forex na ku bet ni baba mmoja kabila tofauti.
Wakati una trade anza na kubeti,huko nako hakuna boss,usisahau jambo jingine biko,hainaga boss aiseee.
Utatajirika fasta.
Ahsante nimemaliza kushauri.
 
Moja Kati ya reply bora kabisa kuwahi kutokea jf [emoji3][emoji3][emoji3]
Hamna jibu Bora hapo

Betting na forex zinatofautiana kwa namna hii
Zote Ni probability ndio lakini

1. ku bet Kuna match zenye high probability ya kushinda na zenye low probability
Ila wenye kampuni wanakuweka wewe always kwenye disadvantage kwa kupunguza rewards kwenye zile match zenye high probability

Mfano Bayern Munich vs Arsenal Ina probability kubwa ya Bayern kushinda, Ila wenye kampuni wanaweka rewards sana kiasi kuwa ili upate hela ya maana labda uweke millioni kadhaa, ambayo ni disadvantage kwa mchezaji

2. Kwenye forex kuna setup zenye high probability ya kupiga pips pia (Kama unajua forex utaelewa hili) lakini tofauti rewards zake hazipunguzwi kisa setups Ina high probability


3. Forex ni biashara ambayo ipo free, Kuna pairs nyingi za ku trade, Kuna brokers ambao wapo regulated, kusema benki zi control movement ya fedha ni ngumu kwani wapo players wengi Sana ambao ku collude Ni ngumu, mfano, Corona virus ilivyotokea Kuna fedha zilishuka na nyingine kupanda kutokana na factors ambazo zinajulikana, Sasa hapo hakuna benki ambazo zingeweza kuungana ili zizuie hiyo movement

4. Forex una muda wa ku practice kwenye demo kadri utakavyo, na ukijiridhisha winning ratio yako Ni kubwa unaweza kuweka hela, Kama sio unaweza kuacha, so mpaka mtu uliwe hela utakuwa umekosa tu kufuata kanuni simple tu
 
Una mda gani kwenye forex, tuanzie hapo!
 
Pips si ndio hela mkuu
Ni sawasawa na kumwambia tajiri wa mabasi kwamba wewe angalia tu basi lako linatumia mafuta litre ngapi ila usiangalie bei ya lita ya mafuta! KATIKA FOREX NO PIPS WITHOUT MONEY AND NO MONEY WITHOUT PIPS. BOTH PARAMETERS ARE IMPORTANT😀 😀 😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…