Wadau mnatumia mbinu gani kupambana na matangazo kwenye Android Phones?

Trubarg

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2020
Posts
4,388
Reaction score
7,223
Habari wadau,

Matangazo kwangu mimi yamekuwa kero kubwa sana. Yaani huwezi fanya jambo bila kukutana na adds, apps ambazo haina adds ni Whatsapp, Insta na X. Zingine kufungua kabla hujafanya lolote lazima ukutane na tangazo kama siyo video basi pop ups. Video zingine zinaenda Hadi dakika kadhaa.

Wadau nyie mnawezaje kuyazuia haya matangazo ambayo hayatarajiwi?
 
Mimi ni team android na simu yangu haina matangazo.
Fanya hivi kwanza acha kutumia chrome browser tumia browser zingine kama mimi natumia opera gx

Pili kuna apps kama N, phones, palm store hizo zote zitoe.
 
Hizo zote sina
 
Kama simu yako ina support Private DNS weka hii domain dns.adguard-dns.com kisha SAVE! Hii domain ya DNS ina block 99% ya matangazo ya Google huitaji AdBlock.

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…