Ukikutana na wafanya tathmini wa kurasa za majarida au vitabu na namna binding itakavyofanyika watakuelewesha vizuri, inabidi kujua aina ya binding kama itahitaji single paper au folding paper. Kwa idadi ya page unazosema nadhani kutumia stitching ni bora na ni gharama nafuu zaidi.
Hivyo basi kama binding itafanyika kwa stitching, means stepple stitching, basi jarida lako litakuwa na kurasa 32. Inategemea na ukubwa wa jarida lako na mikunjo. Inawezakana ikachapwa katika karatasi mbili au nne.
Mkunjo mmoja kurasa 4
Mikunjo miwili kurasa 8
Mikunjo mitatu kurasa 16
Mikunjo minne kurasa 32
Karatasi 1 yenye mikunjo 4 utapata kurasa 32
Karatasi 2 zenye mkunjo 3 kila moja itakuwa na kurasa 16 x 2 = 32
Karatasi 4 zenye mikunjo 2 kila moja itakuwa na kurasa 8 x 4 = 32
Mpango huu wa binding ni kwa kutumia stepple machine kwa stitching na ni gharama nafuu ya binding, na huo ndio mchanganua wa kujua mpangilio wa kurasa.
Ukiwasilaina na wataalamu wa publishing kuna fomula za kutengeneza kurasa, ndio unaona wakati mwingine kitabu kinakuwa na kurasa tupu (blank pages) si kwa kukusudia, ila kutokana na mfumo wa utengenzaji hasa kwa mpangilio wa mikunjo.