WADAU MSIACHE KUNUA HIKI KITABU KIITWACHO IJUE ISRAELI, UPATE UCHAMBUZI WA MATUKIO YAKE YOTE MUHIMU YA KIHISTORIA KUHUSU ISRAELI. ANGALIA HUU MUHTASAR

Raphael Mtui

Member
Joined
Nov 26, 2024
Posts
78
Reaction score
204
Katika kitabu hicho, waandishi wamejikita kujibu swali linaoulizwa mara kwa mara la Israeli inatuhusu nini sisi Wakristo? Kuna ulazima gani wa sisi kujifunza na kuifuatilia Israeli? Na je, Israeli kuwa taifa teule ina maana uteule wao unatokana na wao kuwa watu wema wanaompendeza Mungu?

Katika kitabu hiki, wamekuwekea ile miujiza mikubwa mitano ya kivituko iliyotokea hekaluni kuwaashiria Wayahudi wanakosea kwa kuweka imani kwa hekalu badala ya kwa Yesu. Usiache kujua mambo ya ajabu yaliyotokea hekaluni na baada ya Yesu kusulibiwa na kuleta fadhaa kubwa kwa Wayahudi wakati ule kabla hekalu halijabomolewa na Warumi mwaka 70AD.

Pia, waandishi wamekuonesha mahesabu kamili ya unabii wa Ezekiel jinsi alivvyotabiri Israeli itapata uhuru mwaka 1948, na tukaeleza kwa upana ile stori ya kusisimua ya jinsi mambo yalivyoenda ile tarehe 14 May walivyopata uhuru. Lile tamko rasmi la uhuru wa Israeli hatimaye limetafsiriwa kwa Kiswahili, na kuwekwa ndani ya kitabu hiki.

Hali kadhalika wamekupa stori yote ya maajabu jinsi Israeli ilivyofutwa kwenye ramani ya dunia kwa miaka karibu 2000 na bado ikazaliwa tena, na tena kuwa simba tishio. Tumeorodhesha vita vyote walivyopigana tangu wapate uhuru na bado wakashinda kwa kishindo licha ya kushambuliwa na muungano wa majeshi makubwa.

Katika kitabu hiki utapata historia nzima ya taifa la Israeli tangu pale kwenye tukio la kitabu cha Mwanzo 12 Ibrahimu alipoitwa, historia hiyo ikaja hadi mwaka 2024. Historia hii ya kusisimua sio ya kukosa kabisa, kwa kuwa matukio yote muhimu yaliyotokea kwa Israeli yameorodheshwa.

Pia, utapata kwa undani historia tukufu ya Hekalu la Yerusalemu, hekalu la kwanza lililobomolewa na Nebukadreza na la pili lililokuja kubomolewa na Warumi mwaka 70AD.
Kitabu kimeangazia kwa nini Wayahudi hawajafanikiwa kujenga hekalu lingine mpaka leo, vikwazo vya ajabu walivyokutana navyo wakati wanajaribu kujenga hekalu la tatu ikiwemo moto uliokuwa unatokea ardhini na kuwachoma wajenzi kiasi cha kufanya ujenzi usimame. Pia, tumeeleza kwa undani juu ya michakato yote iliyofanywa na Waisraeli ya kupata ng'ombe mke mwekundu asiye na kipaku ambayo imefanyika dunia nzima pasipo mafanikio.

Lifahamu kundi hatari la kigaidi la Kiyahudi lililoitwa Wazelote ambalo lilichangia Israeli kufutwa kwenye ramani kwa karibu miaka 2000! Fahamu lilivyozaliwa na lilivyofanya mauaji na ukatili kiasi cha kuisogeza Israeli kutimiziwa unabii wa machozi yaliyodumu kwa milenia mbili.

Pia utapata kujua kiundani namna ya kutofautisha Wasamaria na Wayahudi. Fahamu chanzo cha Wasamaria, na walikopotelea na upate kujua vizuri makundi hayo.

Kitabu hiki kina kurasa 142, kwa shilingi 15,000 unakipata kama soft copy.

Wasiliana nami kwa namba 0762731869, piga au whatsapp.

Raphael Mtui.
 
Kwanza kabisa, thibitisha Mungu yupo.
 
Kwanza kabisa, thibitisha Mungu yupo.
Biblia yenyewe kuanzia Mwanzo mpaka Ufunuo haina andiko hata moja linalojaribu kuthibitisha kwamba Mungu yupo, sembuse mimi!

Ushahidi wa uwepo wa Mungu upo wazi mno kiasi ambacho hata Biblia haijawahi kutafuta kuthibitisha kuwepo kwa Mungu.

Sana Biblia imesema wazi kuwa MPUMBAVU tu ndiye anayeweza kusema hakuna Mungu:

Zaburi 14:1 (KJV) MPUMBAVU amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.

Zaburi 53:1 (KJV) MPUMBAVU amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema.

Mpumbavu maana yake ni mtu anayejua ukweli kabisa lakini anafanya tofauti na ukweli huo.

Yafuatayo ni mambo machache yanayothibitisha uwepo wa Mungu.

1)Uumbaji. Kila mwanadamu amezaliwa akijiuliza nini chanzo cha kila kitu.

2)Dhamiri. Kila dhamiri ya mwanadamu huwa inamwambia wazi kuwa kuna Mungu. Hata asipomjua Mungu ataabudu hata jiwe, mbuzi, jua, mti, mlima.

Kwenye dhamiri ndio tunapata kitu chaitwa Imani ya Asili (Natural Faith) ambapo kila mtu anaamini tu kwamba kuna Mungu ahata kama anabisha.

3)Maandiko: kwa jinsi yalivyovuviwa.

4)Yesu Kristo: naye ni uthibitisho kuwa Mungu yupo.

5)Maisha ya Wakristo: wanapomwamini Yesu na kuokoka, maisha yao yanabadishwa na kila mtu mtaani anajua hakika kuna Mungu, kwa jinsi walimjua mtu kabla hajaokoka.
 
Mpaka sasa hujathibitisha Mungu yupo.

Umetajataja imani yako ya kidini na kutoa logical fallacies za argument from authority na ad hominem.

1. Kujiuliza chanzo cha kila kitu si uthibitisho Mungu yupo. Ni kuthibitisha hatujui chanzo.

2.Si kweli. Watu wengi hawakubali uwepo wa Mungu, wakiamua kuabudu chochote hilo halimaanishi Mungu yupo.

3. Hoja ya maandiko ni logical fallacy ya argument from authority. Maandiko yenyewe yamejaa contradictions ambazo huwezi kuzitatua.

4. Hata huyo Yesu Kristo huwezi kuthibutisha ni Mungu.

5. Ukristo una ujinga na uongo mwingi sana hivyo hauwezi kuwa uthibitisho wa kuwapo Mungu.

Hujathibitisha Mungu yupo.
 
Hii ma-fallacy arguement nimecheka sana!

Basi nakubali kuishia hapo kwa mjadala huu mkuu.
 
Hii ma-fallacy arguement nimecheka sana!

Basi nakubali kuishia hapo kwa mjadala huu mkuu.

Unacheka lakini umezielewa hizo fallacies?

Umekubali kuishia hapo au umekubali umeshindwa kuthibitisha Mungu yupo?
 
Hakuna Taifa teule hapo. Hao ni wahuni tu wamekusanyana Ulaya na Amerika, halafu wakaenda kutengeneza himaya yao ya kuua na kudhulumu wanyonge haki zao huko Mashariki ya Kati.
 

Leta profile ya Mwandishi kabla ya namba ya simu!
 
Amina...
kwa jinsi walimjua mtu kabla hajaokoka.
 


Kiburi cha uzima...Au u wakala wa side 2...Siku inakuja utalia na kusaga meno
 
Kiburi cha uzima...Au u wakala wa side 2...Siku inakuja utalia na kusaga meno
Kulia na kusaga meno nako ni uthibitisho kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Katika ulimwengu ambao Mungu huyo yupo, hakuna kiumbe chake chochote kitakacholia na kusaga meno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…