Kwa 'idea' ya Mr. Kuku ilivyo ni kama kitu kinachoitwa 'Crowdfunding'.. yaani anatokea mtu anakuja na 'idea' yake ya biashara halafu wanatafuta watu wengi(wawekezaji) ambao watatoa fedha ili kuiwezesha hiyo biashara na kunakuwa na 'platform' ya kuwaunganisha ambayo ni biashara ya kuku.
Ukishawekeza fedha zako na wao(Mr. Kuku) wataanza kufuga kuku na kuuza na wateja wakubwa wanakuwa hao hao waliowekeza pamoja na wengine. Kwa hiyo ijapokuwa umewekeza fedha lakini unalazimika kununua kuku, nyama ya kuku, mayai,vifaranga ili kuharakisha faida. Ina maana ikipatikana faida mtagawana lakini ikitokea hasara mtagawana pia.
Kwa nchi zilizoendelea inaaminika sana.
Hapa Tanzania ina changamoto sana hasa kwa wawekezaji kwani:
- Hupewi vitabu vya fedha('Income stat. & balance sheet') kujiridhisha kama faida inapatikana.
- Gharama ya uhakikisho ni kubwa('Due diligence costs').
- Gharama ya ufuatiliaji wa mradi('monitoring') siku kwa siku ni kubwa kwa mwekezaji.
- Taarifa zinazotolewa ni za kuvutia na za upande mmoja('information assymetry').
Kwa hiyo miradi kama hii ni rahisi sana kugeuka na kutumika kama vichochoro vya kutakatisha fedha au 'Ponzi Schemes' kama Serikali haitaingilia kwa kuweka kanuni zinazoeleweka ikiwemo kuweka sehemu ya fedha za uwekezaji kama dhamana Benki Kuu.