Hizi ishu ukiziwahi mapema unapiga pesa, ila kadri watu wanavyozidi kuwa wengi ndipo hatari inapokaribia, na hili linasababishwa na sababu kuu mbili, ya kwanza ni kampuni husika kuja kushindwa kuwalipa the so called wawekezaji, endapo kutakuwa na load kubwa. Na sababu ya pili ni kuchongewa serikalini, kuna baadhi ya watu hawatopenda au kufurahishwa na hiyo aina ya investment hasa financial institutions coz watu wanawakimbia na kwenda kuinvest huko upatuni, ikifikia hali hiyo ndipo wanapoenda kuripoti kwa mamlaka husika serikalini na uchunguzi unaanza na mwisho wa siku kampuni husika inafilisiwa, na watu kuanza kulizwa.
Ila early birds wanapiga mkwanja aise..na ndo hivyo ukishazivuna za kutimiza malengo inabidi uwapige na chini ili dhoruba lisikufike.