Wadau nani anajua bei za haya magari Afrika Kusini?

Sasa gari la 2017 toyota Fortuner bei rand 250,000/: ambayo ni 38,750,000/: kule be forward utakuja mil.50 fortuner la japan, bado Ushuru , kumbe africa kusini ukiwa na taarifa sahihi unapata gari bei nzuri sana na hakuna garama kubwa ya kusafirisha kama ilivyo japan, kwa sasa Africa kusini ndo pa kwenda kununua gari za kazi kama hilux kwa sisi wafugaji , Japan wanauzia umaarafu ILA south africa ndo Habr ya mjini kwa wale risk taker.

Sent from my TECNO B1g using JamiiForums mobile app
 
Inaweza range kwa bei gani kwa makisio?
 
Kaka mimi naomba nipate mawasiliano yako, nahitaji kuja huko mwaka huu July
 
Tunashukuru sana kwa haya maelezo , binafsi nimependa maelezo yako , na yamekuja wakati muafaka Asante sana ubarikiwe

Na pia kama hutojali niangalizie Mazda CX 5 petrol engine ya 2013 zinapatikana kwa bei gani SA.
 
Tunashukuru sana kwa haya maelezo , binafsi nimependa maelezo yako , na yamekuja wakati muafaka Asante sana ubarikiwe

Na pia kama hutojali niangalizie Mazda CX 5 petrol engine ya 2013 zinapatikana kwa bei gani SA.
Ukitaka kuangalia kitu chochote mitandao ya SA andika tuu Mazda CX 5.co.za code yao ni Co.za hata kitanda au chochote utaenda kwenye mitandao yao ila usifanye malipo yeyote huko pana utapeli sana rate yao zidisha na 140 mpaka 145 ndio iliyopo kwa sasa ingawaje hiyo mazda zipo nyingi ni Ford hao unaweza kupata rand 130,000 kuendelea ukizunguka sana unaweza kupata hata chini ya hapo wauzaji SA wanatofautiana sana bei....ukitaka kuja ili ufanyiwe mchakato wote sawa tu pia...
 
Nashukuru sana nimepata elimu , itabidi nije SA nisafishe macho , ila miji mizuri ambayo uhalifu ni mdogo ni wapi , maana sisi wengine tunasikia mara fulani kapigwa chuma ,
 
Anaesema gari za bondeni ni lonya hana akili kwakua hata hizo za japan wanaziservice ndio watuuzie ukifondoka bondeni unajipimia gari gani unataka mbona watu wanauziwa malonya from japani. Kila mtu anakitu chake anakijua mm hata leo nikitaka kununua gari lazima nimcheki mwanangu anipe muongozo.
 
Daah gari zenyewe ni hizi hapa...
 

Attachments

  • 20230418_154249.jpg
    481.9 KB · Views: 12
  • 20230418_155109.jpg
    377.3 KB · Views: 7
  • 20230418_152350.jpg
    513.4 KB · Views: 10
  • 20230418_152237.jpg
    481.4 KB · Views: 10
  • 20230213_143756.jpg
    814.9 KB · Views: 15
  • 20230213_143743.jpg
    624.2 KB · Views: 9
  • 20230213_143751.jpg
    780.8 KB · Views: 17
  • 20230208_150447.jpg
    805.2 KB · Views: 9
  • 20230208_150607.jpg
    812.8 KB · Views: 12
Mpaka nimemeza mate lakini sisemi ni kwa nini! Nashukuru sana. Nimeshajua pa kuanzia!
πŸ™πŸ™πŸ™
Nilowahi nunua Ford Bantam SA mwaka 2013 nimekuja kuuza 2022 nilichobadili ni Tairi na alternator nayo ilimwagikiwa na Hydrolic ya kwenye power Sterling pana mfugaji kila nikikutana nae alikua anaomba nimuuzie nimemwachia anataka kingine maana Kigali hakitumii mafuta mengi ni cc 1300 kina speed 240 harafu gear 6 pamoja na reverse yake kinatembea balaa na balance ipo hicho Kigali ndio Kigali nilikua nikitoka SA hata nikae muda gani kinawaka haraka kuliko gari zote...
 
Hilux kiukweli japan wanatupiga bei kubwa halafu Gari zenyewe ambazo tunahitaji ndo hizo 2005 mpaka hadi 2009 unatoa mpaka milioni 60 na kitu daah.

Isanga Family be blessed yani umenifungua maana ninashida kweli kumbe sasa ni focus na soko la SA labda maumivu yatapungua walau Hilux kulingana na mambo ninayofanya ni lazima wala siyo ombi wala hobby ni lazima ili mambo yaende[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nitake nisitake majukumu ndo yanahitaji hiyo gari and the like.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…