Wadau nani anajua bei za haya magari Afrika Kusini?

Sorry kaka nitakuuliza mfano ushuru wa hyo ya 2010 ushuru wake utakuwaje?utakuwa wa SADC au kama tu wa japan?
Unakua wa SADC kama gari ni mpya inapungua sana kwenye VAT ila kama sio mpya haitatofautiana na Japan ila port charges na taka taka zingine za bandari hazitakuwepo..
 
Sasa Mercedes Ni maker au model ? We mtu alikwambia Toyota Ni sh ngapi utamjibuje
 
Nimeangalia online naona bmw x3 2014 hadi 2016 wanauza rand 250,000 na kuendelea. Naona zipo juu kama Japan au wauzaji wa mitandaoni wanatulangua sana?
BMW na VW zipo ghari SA maana zina soko kubwa pia ila hao jamaa wa mtandaoni sio wa kufanya nao biashara wengi matapeli...SA ukinunua gari mara moja kwa kufika eneo la tukio hayo mengine ndio unaagiza tu humu wapo wengi wametapeliwa na Wasauzi wakishatapeliwa ndio wanakuja inbox ila hawaji kuuliza kabla hawajafanya malipo hicho ndio kinachonishangaza..
 
Asante sana kwa ushauri, nlikuwa naangalia bei online ili nijue najiaandaa na sh ngapi ila kununua itabidi nisafiri
 
Nimeangalia online naona bmw x3 2014 hadi 2016 wanauza rand 250,000 na kuendelea. Naona zipo juu kama Japan au wauzaji wa mitandaoni wanatulangua sana?
BMW X3 2014 kwenda juu chungulia singapore hapo.
 
Nimeona ni cheaper than Japan. Ila reliability ipoje, maana nasikia Singapore hamna ukaguzi kama Japan
Gari zao ni nzuri ukipata kwa dealer reliable. Nilinunua 2021/22 sioni shida yoyote. Japan kukariri tu. Ukiingia hara be forward wana sehemu ya gari za singapore.

Ila wengi wanasema Singapore wanachezea odometer na kufanya interior design kabla ya kuuza gari.

Kwangu niliona tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…