Wadau naombeni ushauri jinsi ya kuwekeza hizi shs. 10,000,000

Lima matikiti, kwa kila heka unapata faida ya milioni 2 mpaka 3.5. na yanachukua siku 60 mpaka kuvunwa. Mimi nina eneo linalofaa kwa kilimo hicho Kigamboni KM 24 kutoka ferry na panauzwa kwa milioni 1 kwa heka.

Mkuu nimevutiwa na hili wazo. Naomba ufafanuzi zaidi kwa manufaa ya wale wote tunaopenda kuanza ili tufahamu kiundani kabla ya kuja kukutafuta ili kununua shamba.

Gharama yote kwa eka kuanzia kununua shamba hadi mavuno naweza kutumia sh ngapi kwa wastani? Nikishauza matikiti naweza kupata sh ngapi? Je naweza kulima matikiti miezi yote 12 kwa awamu kama nimenunua eka zaidi ya moja na nikavuna kila mwezi bila tatizo au kilimo ni kwa msimu tu? Naomba kwanza unisaidie kwa haya maswali kwanza mengine tutatafutana maana nina shauku kubwa sana ya kuanza kilimo hiki.
 
Duka la spea kwa milioni 10?!!!
Sidhani kama mtu unaweza kuwaza kuanza duka la spea bila kuwa na milioni mia kadhaa...
 
Duka la spea kwa milioni 10?!!!
Sidhani kama mtu unaweza kuwaza kuanza duka la spea bila kuwa na milioni mia kadhaa...

vipi kuhusu spare za pikipiki? sio lazima duka liwe kuubwa, kwa kuanzia tu, mtaji sh ngap ndugu
 
vipi kuhusu spare za pikipiki? sio lazima duka liwe kuubwa, kwa kuanzia tu, mtaji sh ngap ndugu

It greatly depends where you are... kama uko huku mjini ambako competitors wako ni wakubwa sidhani kama utamake
 
 
Kama hujielewi bora ukanuue hisa ukiwa unawaza nini cha kufanyia.

Spare parts zinalipa sana, kuanzia za pikipiki au magari, profit margin yake ni 500%. Ukiweza kuzifuata dubai utakuja kusimulia.

kuhusu spare za pikipiki ndugu, nikitaka kuanza kabla ya kwenda huko dubai mtaji minimum sh ngapi? maana location ni mkoani sio dar
 

Matikiti ni zao lisilopendelea maji mengi, kwa hiyo unapolima ni vyema
kuepuka misimu yenye mvua nyingi, zaidi ya hapo unaweza kulima misimu
yote.
Kuhusu gharama mpaka kuvuna andaa laki 4 kwa heka kwa ajili ya palizi,
upandaji, madawa na kumlipa mmwagiliaji.
Baada ya kuvuna, kwa kila heka utapata faida ya milioni 2 mpaka 3.5
baada ya kutoa gharama za mwanzoni(initial costs).
 
heka 1 ya matikiti inakuwa
na wastani wa miche mingapi mkuu? kila mche unakuwa na matikiti
mangapi?

Heka 1 inapandwa wastani wa matiki 1000 na kila mche unatoa tikiti 1 mpaka 10.
Mauziano hufanyika shambani kwa mnunuzi na muuzaji kukubaliana bei ya kuvuna heka nzima. Lakini hilo haliondoi wazo la muuzaji kuyavuna matikiti na kuyapeleka mwenyewe sokoni kama Buguruni, Temeke, Ilala, au Mabibo na kuyauzia huko.
 
kuhusu spare za pikipiki ndugu, nikitaka kuanza kabla ya kwenda huko dubai mtaji minimum sh ngapi? maana location ni mkoani sio dar

Tafuta kama mil 3-5, anza na zile spare ambazo zinahitajika sana,
 
Lima matikiti, kwa kila heka unapata faida ya milioni 2 mpaka 3.5. na yanachukua siku 60 mpaka kuvunwa. Mimi nina eneo linalofaa kwa kilimo hicho Kigamboni KM 24 kutoka ferry na panauzwa kwa milioni 1 kwa heka.

No yako mkuu, mi nahitaji
 
Lima matikiti, kwa kila heka unapata faida ya milioni 2 mpaka 3.5. na yanachukua siku 60 mpaka kuvunwa. Mimi nina eneo linalofaa kwa kilimo hicho Kigamboni KM 24 kutoka ferry na panauzwa kwa milioni 1 kwa heka.

Jerry no plz
 
Duka la spea kwa milioni 10?!!!
Sidhani kama mtu unaweza kuwaza kuanza duka la spea bila kuwa na milioni mia kadhaa...

Acha kumtisha bwana! Hii ndo shida ya wa-Tz hatujui kuanza kidogo kidogo, tunataka tukianza tu duka hilooo misifa mji mzima!! Nafikri katika hili anaweza kuanza kidogo kwa kuangalia zile spea muhimu na uzuri kwa vile hatarajii hii fedha kuwa anaitumia kwa kula naamini ataenda! Hapa achotakiwa kufanya ni kuangalia ni spea zipi zinatoka haraka! biashara nyingine ni duka la vifaa vya ujenzi vile vidogovidogo, hii inalipa sana tu hasa ukipata site nzuri.
 

Mke wa Mkuu, umetoa ushauri mzuri sana! Kila siku mahitaji ya vitu hivyo yanaongezeka lazima atafanya biashara tu! Hapo pa kwenda Dubai inakuaje mkuu? Vifaa vya ujenzi inatakiwa mtu uanze na mtaji kiasi gani? Au hivyo vya umeme? Dubai na Hong Kong wapi panalipa?
 

Hongkong hapana china ok lakini lazima uwe na agent wa kukusaidia na ujue kuchague vitu vilivyo bora china kuna vitu rahisi sana na vitu ghali na quality tofauti watu wanavyodhani dubei ni pazuri mzigo unafika kwa muda mfupi pia unapata vitu imara hasa ukienda sehemu moja inaitwa. Raslihema sehemu hiyo ndio inaviwanda vingi vitu vya china dubei utapata dragon mart kuna maagent wa viwanda vya china dubei kwa sasa hotel ziko juu kidogo sio kama zamani ila china hotel kiasi nafuu mtaji wa chochote unategemea research yako wewe mwenyewe ila ushauri usivamie biashara kwa mtaji mkubwa sana anza kidogo kisha ongeza mtaji kufwatana na soko lako though my experiance
 

Ok...
Endelea tu kumpotosha mwenzio lakini hakuna mfanyabiashara anayeweza kumshauri mtu aanze biashara ya spea za magari kwa sh m10... never.
Fremu inayoweza kubeba biashara ya spea hapa mjini sio chini ya laki 2 kwa mwezi... akipata msamaria akampa kwa miezi sita (wengi ni mwaka mmoja siku hizi), ina maana m1.2 imeondoka. Akiweka mashelvu, meza, nk... laki nane zimeondoka, amebaki na m8. Akienda TRA na halmashauri kusajili biashara, laki 2 zimeondoka. Huyu ni mfanyakazi, itabidi aajiri muuzaji, ambaye atalipwa sio chini ya laki kwa mwezi... Ina maana akiwa makini sana ataanza biashara yake kwa mali ya sh m7 na ushee... Milioni 7 Spea? Na unatarajia watu waje dukani kwako, uuze average mali ya laki tatu kwa siku (ili upate faida ya 30,000-40,000) ili mwisho wa mwezi uwe na angalau faida ya milioni moja, ambapo ukilipa kodi laki na nusu, mfanyakazi; laki, umeme; elfu 20, usafi marekebish nk, halafu riba ya benki (around elfu 50) ubaki na faida yako...

It never works that way mkuu...

Zipo biashara nyingi ndogo ndogo za kufanya na m10 kutokana na eneo alilopo lakini sio duka la spea...
 

Hao maagent wenyewe ndo wana vidhaa au ni madalali kama wa bongo? Ulipaji wa ushuru nao umekaaje?
 
Ma agent wa china wanakusaidia kupata kitu hakika ulichochagua. Unaweza kuweka order yeye anakuwa anafwalia na kuhakikisha ndio kitu halisi maana wachina wajanja sana unaweza kuchagua kitu bora ukalipia ukiondoka tu unawekewa vitu vibovu sio wabongo ni wa china na wengine wanakusafirishia mpaka dar swala la ushuru sasa fanya utafiti mwenyewe mimi nimeishia hapo kuna kichwa wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…