Wadau naombeni Ushauri wa Haraka kwani Ajira Imekuwa Ngumu

Wadau naombeni Ushauri wa Haraka kwani Ajira Imekuwa Ngumu

RC.

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2012
Posts
444
Reaction score
41
Nina wazo la Biashara, ambalo natamani nilifanye lakini sijajua mtaji wake ni Tshs ngapi ili niweze kuifanya biashara hii kwa ufanisi na kuwapa wateja wangu ile kitu roho inapenda, wazo lenyewe ni:

Nataka kufungua ukumbi wa kuonesha mipira ligi mbalimbali za ndani na nje ya Tanzania hususani ligi za ulaya! na nina mtaji wa Tshs 1,500,000/=,mchanganuo wake unakuwaje hapo, TV tayari ninazo mbili.

Je kwa hawa supersport garama zao inakuwaje?

Je pesa hii inatosha kuanzisha mradi/biashara hii ninayoipanga, naombeni ushauri wenu wadau ili niweze kujikwamua na tatizo la ukosefu wa ajira?

Naomba kuwasilisha.
 
Bro ikiwa total uko NA rhizome match nakushaur ukuwe risk taker Lila kiting no kujaribu man
 
Bro ikiwa total uko NA rhizome match nakushaur ukuwe risk taker Lila kiting no kujaribu man
Hivi huyu nae yumo?maana hakuna hata moja aliloeleweka.

Biashara hii inalipa ila inategemea na maeneo uliyopo au unapotaka kwenda kufungua huduma hii.
 
Frame, mabenchi, umeme, wirin, subwoofer, PVR decoder, na subscription fee. Huenda ikatosha mkuu kama ukikaza.
 
Inaalipa sana kamanda ila ni lazima uzingatie baadhi ya mambo kwa mfano;

Eneo unalotaka kufungua biashara yako kuna wateja kwa maana kamili ya wapenda soka?
Na kama wapo wanatazama wapi hizo mechi?
Ukishafahamu hayo nenda kwa hao wanaoonesha mipira ambao wapo jirani ufanye kautafiti kidogo kuhusu ubora wa huduma zake na nini mapungufu yake then uyachukue kama changamoto yale mapungufu fanya kila uwezalo yasitokee kwako na yale mazuri yaboreshe zaidi hakika utafika unapotaka..

Kwa huo mtaji wako unaweza kutosha kama tayari una ukumbi na hizo TV mbili lakini kama unategemea hela hiyo hiyo hadi kujenga ukumbi inaweza kukuletea shida kwa sababu mwezi wa kwanza usitegemee kupata faida kubwa so utahitajika kutoa hela mfukoni kwenda kulipia dstv kua makini usitumie hela zote ukitegemea ukipata faida ndo utalipia yote ya yote kila la kheri mkuu.
 
Back
Top Bottom