Nilipata tatizo la chuma ulete kwenye biashara ya duka la vyombo Makuburi Dsm mwaka 2016 aisee nilikua sioni faida na mtaji ukawa unalika balaa.
Nilishauriwa na wasamalia wema wa mtaa ule walioona duka langu lililokua mwanzo limejaa likawa linaporomoka siku hadi siku. Nikaunganishwa na mtaalam.
Ni dawa flan ivi ya maji nilipewa na Mzee Lugendo wa kijiji flani kinaanzia na herufi "K" wilaya ya Handeni ...aisee ni kiboko ya chuma ulete. Na akanielekeza siku nyingine kwenye biashara yoyote nikipata changamoto ni Kwato tu au mfupa wa mnyama flan unatwangia na majani ya mti flan maarufu saana na maji then unamwaga kwenye mlango wa duka au nyumbani kwako kama mstari flani afu unapita kwa kuruka then endelea na mishemishe