Wadau wa elimu tuliangalie hili kwa jicho pevu.

Wadau wa elimu tuliangalie hili kwa jicho pevu.

ADRIAN

Senior Member
Joined
Dec 31, 2012
Posts
113
Reaction score
27
Ndugu Watanzania nawasalimu.



Leo naomba tubadilishane uzoefu juu ya utaratibu wa uendeshaji wa vyuo vyetu mbali mbali hapa nchini kwetu.


Kwa leo nitaangazia chuo cha TIA (TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY)



Kwanza nawapongeza walimu na wsimamizi wote wanaohusika na uendeshaji wa chuo hiki kwani kwa kiasi Fulani kimeonyesha mafanikio makubwa katika kutengeneza ajira nyingi kwa watanzania hasa wenye ufaulu wa chini wanaomaliza kidato cha nne nk.

Lakini pamoja na pongezi hizo, chuo hiki naona sasa kimeanza kujaa UKABURU WA KIUONGOZI DHIDI YA WATEJA WAKE.

Katika vyuo vingi hapa nchini kuna utaratibu ambao nadhani ni mzuri ambao ningependa chuo hiki kiuzingatie katika kuwahudumia wateja wake. Utaratibu huo nitaueleza katika maeneo mawili ambayo ni:-


  1. ULIPAJI WA ADA
  2. UFANYAJI WA MITIHANI.

1. ULIPAJI WA ADA.

Kila chuo kina mihula miwili kwa mwaka. Ambapo muhula wa kwanza mwanafunzi hutakiwa kulipa ada ya masomo kwa kiwango cha asilimia 50% ya ada yote ya mwaka. Kwa mfano, kama ada ya mwaka ni milioni moja, mwanafunzi hutakiwa kulipa lakini TANO (500,000) ndipo aruhusiwe kufanya mtihani wa kumaliza mhula wa kwanza.


LAKINI chuo cha TIA ni tofauti kabisa kwani wao wanalazimisha wanafunzi wao kulipa asilimia SABINI 70% ya ada ya mwaka kabla ya kumaliza mhula wa kwanza na anayeshindwa kufikia asilimia hizo haruhusiwi kufanya mitihani. Kwa mfano wanaosoma cheti(CERTIFICATE) ambao ada yao kwa mwaka ni laki SABA NA NUSU 750,000/= wanatakiwa kulipa 580,000/= kabla ya kufanya mitihani ya muhula wa kwanza. Na mhula wa pili watamalizia laki na Sabini tu 170,000/=.



Kwa hili naona siyo haki kwa wanafunzi na wazazi wanaohusika na utafutaji wa ada maana tunawakandamiza sana. Ikumbukwe hapa nusu yam hula wa kwanza ni 375’000/= ambazo ni sawa na asilimia 50% ya ada ya mwaka wa masomo na ambayo mzazi anaweza akaimudu na ukizingatia kipato cha watanzania wengi ni kidogo sana.


Lakini cha kusikitisha ni kwamba, mwanafunzi anayeshindwa kufikia kiwango cha laki 580,000/= anazuiliwa kufanya mitihani. Kwa mfano mtu anayelipa laki 350,000/= au 400,000/= hawezi kuruhusiwa kufanya mtihani wa semester ya kwanza ambao kwa mwaka huu utaanza tarehe 20/01/2014. Je hii ni sawa? Kwani mwanafunzi akimaliza semester ya kwanza si atakuja kuendelea na semester ya pili ambapo angeweza kumalizia ada hiyo? Tafakarini jambo hili.


  1. UFANYAJI WA MITIHANI.

Vile vile katika vyuo mbali kuna mitihani mbali mbali hutolewa ili mwanafunzi anayehusika na kozi Fulani aweze kupimwa kiwango cha maarifa, ujuzi na staid alizozipata kabla ya kumaliza chuo. Utaratibu huo ni pamoja na Assignments, tests na semester 1 exams na final exams.

Vile vile kuna mitihani ya wanafunzi wanashindwa kufanya mitihani ya semester 1 au kufanya tests kwa muda ule uliopangwa. Watu hawa hupewa mtihani maalumu (special exams) kwenye semester 2 mwanzo, katikati au kabla ya kufanya final exams ili waweze kuendana au kuwa sawa na wenzao. Vile vile huwa kuna mitihani ya SUPPLEMENTARY kwa wale wanaoshindwa kufikia alama tarajiwa kwa MALIPO MAALUMU.

KINACHONISHANGAZA kwenye chuo cha TIA ni kwamba, ikiwa mwanafunzi aliyeshindwa kufanya mitihani ya kumaliza semester 1 ama kwa kukosa ada au sababu nyingine yoyote na akiwa tayari ameshalipa ada 200,000/=, 300,000/=, 400,000/= na hakufikisha 580,000/= anazuiliwa kufanya mtihani na hataruhusiwa kuendelea na semester ya pili anafukuzwa chuoni hapo.

Mwanafunzi huyu anaambiwa aanze upya mwaka mwezi wa September na ada ya awali haitahesabiwa kwa kisingizio eti WALISHAMHUDUMIA. Hii ni haki kweli???
Kwanini wasitoe fursa kwa wanafunzi hao kufanya mitihani ili waje wadaie ada hiyo kwenye semester ya pili? Au kwanini wasipewe special exams kabla ya kufanya mitihani ya FINAL? Hivi hivi vyuo vipo kwa ajili ya kutoa elimu na ujuzi kwa watanzania masikini? Case study TIA SINGIDA BRANCH.



Nashauri serikali ya chuo hiki ifanye jitihada za kuhakikisha wanafunzi wenzao wanapata haki hizi. Ikumbukwe pia uongozi wa chuo ndio unao miliki vyeti vya wahitimu ambao nilichokishuhudia ni kwamba kabla ya mhitimu kuchukua cheti chake lazima ajaze clearance form kujua kama anadaiwa au la. Sasa kama kuna utaratibu wa kuwalazimisha kulipa ada hiyo yote kabla hata ya kumaliza mwaka na au wanpokuwa wanamaliza kozi, kwanini muwape hizo clearances???

UONGOZI TENDENI HAKI KWA WATANZANIA WENZENU.
 
Back
Top Bottom