Wadau wa mchezo wa draft, Leo Kuna mpambano wa kukata na shoka Ronaldo vs Noel

Mkuu ivi hakuna wadhamini tuweze kucheki kwenye luninga. Sijui kuucheza ila naupenda huu mchezo hasa ukiwakuta mafundi na maneno yao ya shombo na pia hesabu zao kali sana ukisukuma kete moja tu tayari anakumbia limeisha
Kabisa mkuu kuna kete ukikosea tu kwa mafundi wanakwambia limeisha,maana huwa hakuna namna hata ubadilikaje.
 
Hua najiulizaga hivi hawa walio master draft wanacheza draft hili hili lenye jumla ya vyumba 64 au lao linakua lina vyumba 6?

Haya madude ndio maana yalitaka kumuua mangwelele
Ilikuwaje mkuu huyu mangwelele.
 
Kuna bwana mdogo mmoja anaitwa Amos alikimbiza sana Bagamoyo miaka ya 2012-2014 Saiv. Nasikia yupo moro
 
Hata hivyo si mbaya maana ni mtu tu katoa hela yake mfukoni na wao wakaridhia na Tena mareiebisho kidogo kumbe mshindi alikuwa alipata 150k na mwenzake akapata 50k.
Mimi ningekuwa mdau wa mchezo huu ningegharamikia 200k nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…