Wadau wa mchezo wa draft, Leo Kuna mpambano wa kukata na shoka Ronaldo vs Noel

Wadau wa mchezo wa draft, Leo Kuna mpambano wa kukata na shoka Ronaldo vs Noel

Mc PIPI

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2020
Posts
325
Reaction score
442
Wakuu,habari ndiyo hiyo,Leo Kuna mpambano wa kukata na shoka Kati ya RONALDO kutoka DAR dhidi ya NOEL kutoka NJOMBE..

Mtanange huu utakuwa wa mechi 24 ambazo zitapigwa ndani ya ukumbi wa michezo wa SANSIRO uliopo Mjini MAKAMBAKO ambapo mashabiki watajipatia fursa ya kushuhudia mtanange huo kwa kiingilio Cha Tsh. 2000/= tu na mshindi wa mtanange huo atajinyakulia kitita Cha Tsh. 200,000/=.

Mtanange huo unatarajiwa kuanza mnamo saa 10 jioni.

Nipo mbali na eneo la tukio lakini nikiwahi kurudi nitawapa updates lakini nikishindwa updates basi nitawapa matokeo ya mwisho.

UPDATE: FT: Ronaldo 3-1 Noel

MAREKEBISHO YA ZAWADI. Kumbe mshindi alichukua Tsh.150,000/= na mpinzani wake Tsh. 50,000/=
 
Msisahau kuchukua video ya mtanange na sisi tulio mbali tuweze kujionea recorded baadae
Kwa bahati mbaya sipo eneo la tukio lakini mtanage wote utarekodiwa na Kama sijakosea huenda vedio hizo zikapakiwa Hadi U tube.Lakini nikiwahi nitatupia updates za kutosha.
 
Mh hivi vitu atatokea mjanja mmoja na kuviweka kwenye channel yake ya tv apige hela.

Ila huyu Ronaldo nahisi bado siyo hatari sana nishamuona akicheza huyo Noel namsikia tu.
 
Wale walikutana kila mchezo unachukua zaidi ya lisaa kumalizika

Ujipange kununua bundle zito
Saa nzima mchezo mmoja? Ah wanazinguwa waweke time limit yaani hata dk 20 naziona nyingi
 
Basi Leo hii Ronaldo akaja kijiweni petu Kuna mwamba mmoja naye kwenye top 3 katika kijiwe chetu amepewa atafute sare tu wakawekeana bukubuku, kapigwa game zote 8 walizocheza yaani hajapata hata sare moja wakati yeye huyu jamaa ndo anawapaga wenzake sare.
Mh hivi vitu atatokea mjanja mmoja na kuviweka kwenye channel yake ya tv apige hela.

Ila huyu Ronaldo nahisi bado siyo hatari sana nishamuona akicheza huyo Noel namsikia tu.
 
Hakika, maana alichofanyiwa ROLNALDO kwenye ile fainali lazima ajiulize vizuri.
Hawa jamaa wana spirit moja hivi ambayo karibia kila bingwa anayo.

Yani mchezo aliofungwa hua hawausahau, yani akitoka hapo anaenda nyumbani anakupangia kete zote namna jinsi bao lilivyokua.

Halafu anaanza kuifikiria kila kete kwa kila angle ajue wapi alikosea. Akijua basi hapo hapo anaweza akarudi kwa yule aliyemfunga na kumuambia tucheze tena. Hata kama ilikua ni kamari jamaa yuko radhi aweke bondi hata simu

Inawezekana kabisa huyu ronaldo ule mchezo aliofungwa na noel kule kitunda ameufanyia majaribio kila siku na kujiridhisha kua hawezi kufungwa tena au ameuboresha zaidi kiasi cha yeye kupata ushindi
 
dah nmemiss sana draft aisee halafu nilipo sasa hamna mafundi dah, hivi kuna app yeyote ya pc ambayo ni ngumu kweli maana app zote nazopataga naona km ni kwa wale wasiojiweza tu
 
Back
Top Bottom