SMACKDOWN JANA
Baada ya Kevin Owens kuwaandama sana The Bloodline (Roman Reigns,The Usos,Solo Sikoa,Sami Zayn) wiki baada ya wiki, kiongozi wa Bloodline, Roman Reigns anaonekana kukosa imani na Sami Zayn ambae alikua ni rafiki mkubwa wa Kevin Owens.
Ili kuthibitisha utiifu wake kwa The Bloodline, Sami Zayn atatakiwa kupambana na aliyekuwa rafiki yake, Kevin Owens wiki ijayo kwenye SmackDown...
Na pia ili kumaliza chokochoko zote za Kevin Owens zinazoweza kuleta mpasuko ndani ya Bloodline, Roman Reigns ameamua atapambana moja kwa moja na Kevin Owens kwenye Royal Rumble.