Mie huwa nasema miachana na mtu matusi ya nini sasa??
Hiyio ilikuwa siri yake kuwa hampendi mumewe na tena akaenda kufunga nae ndoa na
dini akambadili??
Huyo mdada akili yake si nzuri kwa mtu mzima aliyekomaa kiakili
hawezi kutamka ujinga kama huo tena kwenye vyombo vya habari
Kimsingi anajidhaliliisha yeye anaona yuko sawa hajui watu watamcheka??
ni kweli kabisa
1. akiwa mchumba , hampendi lakini anaendelea
2. kwenye ndoa ambako alipewa semina na hata akaulizwa mara tatu, alikubali akiwa hampendi, hataki kumwacha
3. akakubali kubeba mimba bado hampendi, lakini hamwachi
4. amezaa nae sasa ndo anasema hampendi anamwacha, eti kuna anaempenda.
ni kweli huyu binti hana akili, au anatatizo lingine kubwa. hivi kama hampendi kwanini afunge ndoa, kwanini azae nae?. lakini mimi nadhani wengine wajifunze kwake.Irene hafikirii kuwa kuna uzee, anadhani atakuwa vile alivyo siku zote. wazazi wake wangefanya afanyavyo yeye asingependeza hivyo
mwisho nakubaliana na wewe, kuwa hii tabia ya kutukanana wakati wa kuachana inhaina faida , huu siyo ustaarabu. binafsi ninaweza kukosana na mwenzangu, lakini as long as alikuwa ni mwandani wangu kamwe siwezi kumdhalilisha kwa watu, haijalishi alinitenda nini. kama nina cha kusema nitamwambia yeye. kumvua nguo uliyeshiriki nae mambo makuu ni kujidhalilisha mwenyewe