Wadau wa Sekta ya Tumbaku waichambua Dira wa Dira ya Taifa 2050 na Mpango Kabambe wa Kilimo 2050

Wadau wa Sekta ya Tumbaku waichambua Dira wa Dira ya Taifa 2050 na Mpango Kabambe wa Kilimo 2050

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
WhatsApp Image 2026-09-28 at 13.48.06.jpeg
Bodi ya Tumbaku Tanzania (TTB) imekutanisha wadau wa Sekta ya Tumbaku nchini kwa lengo la kutafakari na kuweka mikakati ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 pamoja na Mpango Kabambe wa Kilimo wa mwaka 2050 (Agricultural Master Plan 2050 – AMP 2050).

Kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya Tumbaku ili kujadili maeneo ya kipaumbele yaliyowekwa katika Dira ya Taifa na AMP 2050, pamoja na kuweka mfumo wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa shughuli na malengo ya sekta kupitia taarifa za robo mwaka.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Tanzania, Bw. Stanley N. Mnozya, amesema kuwa Sekta ya Tumbaku ina mchango muhimu katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya Taifa yaliyowekwa katika Dira ya Taifa 2050 na Mpango Kabambe wa Kilimo 2050.
WhatsApp Image 2026-09-28 at 13.48.05.jpeg
“Uzalishaji, tija, uhifadhi wa mazingira, uwekezaji, matumizi ya teknolojia za kisasa, kuongeza thamani ya mazao pamoja na maendeleo ya rasilimali watu ni miongoni mwa maeneo ambayo sekta ya tumbaku imepewa kipaumbele katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 na Mpango Kabambe wa Kilimo 2050,” amesema Bw. Mnozya.

Alieleza kuwa ili kuhakikisha sekta inatoa mchango unaotarajiwa, kila mdau anatakiwa kusimamia kwa umakini viashiria vya utendaji (Key Performance Indicators – KPIs) vilivyopo katika eneo lake la uwajibikaji na kuhakikisha taarifa za utekelezaji zinawasilishwa kwa kila robo mwaka.

“Kila mdau ana jukumu la kutekeleza maeneo yanayomhusu na kutoa taarifa za maendeleo kwa wakati. Mfumo huu utatusaidia kupima mafanikio, kubaini changamoto na kuhakikisha sekta ya tumbaku inatoa mchango wake kikamilifu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa 2050,” amesisitiza.

Bw. Mnozya ameongeza kuwa ushirikiano wa wadau wote wa sekta ni muhimu katika kufanikisha malengo ya kuongeza uzalishaji wenye tija, kuimarisha ushindani wa sekta, kuvutia uwekezaji, kulinda mazingira na kuongeza mchango wa sekta katika ukuaji wa uchumi wa Taifa.
WhatsApp Image 2026-09-28 at 13.48.09.jpeg
Aidha, amebainisha kuwa Bodi ya Tumbaku Tanzania itaendelea kuratibu utekelezaji wa maazimio ya kikao hicho na kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa viashiria vilivyowekwa ili kuhakikisha sekta ya tumbaku inakuwa sehemu muhimu ya mafanikio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Dira ya Taifa 2050 pamoja na Mpango Kabambe wa Kilimo 2050 vinalenga kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa kuongeza tija, ushindani, uwekezaji na matumizi ya teknolojia katika sekta mbalimbali za uzalishaji, ikiwemo sekta ya tumbaku, ili kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa juu wa kati unaojitegemea, shindani na wenye ustawi endelevu.
 
Back
Top Bottom