Wadau wa Usindikaji tukutane hapa

Wadau wa Usindikaji tukutane hapa

vyakula vingi huaribika mapema kutokana na sbabu mbalimbali ikiwemo, vijidudu, vimeng'enyo au uchafuzi wa aina mbalimbali.
Juisi ya matunda ni kati ya bidhaa ambazo zinahitaji umakini mkubwa ili isiharibike.
vitu vya muhimu vya kuzingatia katika uandaaji wa juisi ni hivi vifuatavyo;
  1. USAFI-usafi wa msindikaji, vyombo na mazingira ni muhimu ukadumishwa ili kupunguza uwezekano wa vijidudu na uchafu kuingia kwenye juisi yako. Vijidudu vinapokuwa vingi husababisha juisi kuharibika mapema zaidi
  2. MATUNDA-matumizi ya matunda mabovu au yaliyoharibika huchangia kwa kiasi kikubwa kuharibika kwa juisi. kuna usemi wa kingereza unasema 'Gabbage In Gabbage Out'...usitegemee kupata juisi yenye ubora kwa kutumia matunda mabovu.
  3. kufuata kanuni za usindikaji kama vile kuchemsha juisi na matumizi ya preservatives. Juisi iliyochemshwa na kufungashwa inaweka kukaa kwenye friji wiki mbili hadi mwezi mmoja bila kuharibika...wakati juisi iliyochemshwa na kuwekewa preservatives inaweza kukaa miezi sita hadi mwaka bila kuharibika.
Preservative inayofaa zaidi kwenye juisi ya matunda ni Sodium Benzoate au Potassium Sorbate.
Na nyuzi joto zinazofaa kuchemshia juisi ni degree 80-90 C, kwa dakika 20.

Mkuu nahitaji msaada wako nahisi kuna issue nimekwama unaweza kunikwamua.....
 
Hivi mfano juice ya parachichi na ndizi kama hizi nzito zinatengezwa majumbani,ukiichemsha haiezi haribika?
 
pilipili ya kupika .... Chachandu inahitaji preservatives gani mkuu?
 
Back
Top Bottom