Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo ameunda kamati malumu kwa ajili ya kufanya uchunguzi na kubaini sababu zinazosabaisha msongamano wa malori katika mpaka wa Tanzania na Zambia upande wa Tunduma ambao umekuwa ukilalamikiwa mara kwa mara na madereva hali ambayo imekuwa kero kwa watumiaji wengine wa mpaka huo.
Chongolo ametoa siku mbili hizo wakati wa kikao cha dhararu kilichowakutanisha viongozi wa Mkoa na forodha pamoja na wadau wa sekta ya usafirishaji kwa lengo la kupata suluhu ya changamoto ya msongamano wa malori katika mpaka huo.
Awali wakiwasilisha baadhi ya changamoto hizo baadhi ya wadau wa sekta ya usafiri wakiwemo wamiliki wa malori,chama cha wafanyakazi wa malori Tanzania na mawakala wa forodha Tunduma na viongozi mbalimbali ambapo wameeleza baadhi ya changamoto zao na kuomba ziweze kutatuliwa.
wasimamizi wa usafirishaji na wadau wa forodha katika mpaka wameeleza utaratibu uliopo na namna ambavyo wamekuwa wakifanya jitihada za kuondoa msongamano huo.