george aloyce
JF-Expert Member
- Aug 22, 2017
- 1,302
- 2,023
"Al Ahly wameturudishia Miquissone ambaye hatukuwapa. Mwanzoni ilitajwa kama amenenepa sana. Ni kweli ungeweza kumuona kabisa akiwa amenenepa. Baadaye ikatajwa kwamba amekata uzito na kweli ungeweza kumuona amepungua uzito."
"Tatizo hata baada ya kukata uzito bado hatumuoni Miquissone tuliyempenda na kumhusudu. Juzi aliachiwa Mpira akiwa peke yake na tena katikati ya uwanja, alikimbia na mpira kwa spidi ambayo yeye alijua yupo kasi lakini kiuhalisia haikuwa ile kasi ambayo sisi tunamfahamu nayo. Akakutwa na mlinzi ambaye alikuwa amemuacha kwa zaidi ya mita 20, ingekuwa kwa kipindi kile wakati ana wasili tungesema ni kwa sababu ya uzito wake, na sasa je? [emoji848]
"Juzi Miquissone aliingia kutoka benchi na tena kwenye pambano gumu la ugenini dhidi ya Singida Fountain Gate. Hakuna shabiki aliyeonekana kulalamika kwa sababu wanajua Kiwango chake kilivyo. Mashabiki wetu ni wanazi lakini sio wajinga, endapo Robertinho angemweka benchi yule Miquissone wa zamani basi angekiona cha mtema kuni. Mashabiki wa Simba hawalaumu kwa sababu wanajua wamerudishiwa Miquissone mwingine."
"Tuendelee kumsubiri Miquissone arudi kwenye ubora wake lakini nimeanza kupata shaka kidogo baada ya kukumbuka stori ya Coutinho. Wakati mwingine Mchezaji akirudi kwenye klabu yake ya zamani anajikuta hawezi kurudi tena kwenye ubora wake. Napatwa na wasiwasi na Miquissone kwa sababu licha ya uzito wake kupungua ila bado kasi yake maamuzi yake hayaonekani Uwanjani"
"Kama Miquissone hatarudi kuwa yule tena basi maisha yatakuwa magumu kwa Simba ambayo muda si mrefu itaingia Uwanjani katika michuano miwili mikubwa ya Afrika. Watu wanategemea kuiona ile Simba ya Chama na Miquissone ikiwa kwenye ubora wake lakini wakati Chama akiwa amerudi vyema baada ya kuchemka Morocco, Miquissone hajarudi kama alivyoondoka."