Wadau walalamikia Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuanza kutumika bila Kanuni wala kutolewa kipindi cha mpito kuruhusu usajili

Wadau walalamikia Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuanza kutumika bila Kanuni wala kutolewa kipindi cha mpito kuruhusu usajili

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Wadau walalamikia notisi ya kuanza kutumika kwa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi bila kutolewa kwa kipindi cha mpito kabla ya kuanza kutumika rasmi kwa sheria.

Notisi ya Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi imetolewa ikionesha tarehe 1 Mei, 2023 imeteuliwa kuwa tarehe ambayo Sheria ya Ulinzi wa Taarifa itaanza kutumika.

Vilevile, Sheria hii inalalamikiwa kuwa na mapungufu makubwa hususani kifungu cha 42 kinachoipa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi uwezo wa kufanya kazi bila kujali sheria nyingine yoyote ya nchi na pia kuipa nguvu tume hiyo kuweza kuingia kwenye jengo lolote linalomilikiwa na mkusanyaji au mchakataji wa taarifa binafsi na kuchukua kifaa chochote chenye taarifa binafsi bila kibali cha mahakama.

IMG_9706.jpeg

Kifungu cha 42(1) sehemu (c) na (d) ambako wadau wanapendekeza iwepo idhini ya Mahakama ili kuhakikisha haki inatendeka.

IMG_9704.jpeg


Kifungu cha 42(3) ambacho kinalalamikiwa na wadau kuwa kitapelekea sheria nyingine za nchi kuvunjwa

sheria 2.jpg


Pia, wadau wamesema Maoni yaliyotolewa kurekebisha Muswada kabla haujawa sheria hayaonekani kwenye sheria na huku Kanuni zinazosimamia utekelezaji wa sheria husika zikiwa hazipo wazi kwa umma.

Mdau mwingine amedokeza: “Sheria itasimamiwa na Tume….. sheria imeanza kabla ya tume kuundwa, hivyo sheria inatekelezwa bila mtekelezaji”

Huku mwingine akieleza “Sheria husimamiwa na kanuni na miongozo; miongozo ililetwa kwa wadau lakini hakuna mrejesho wala nakala ya kanuni husika”
 
MAkubwa , madogo yana afadhali , haya yooote ni kujastifai upuuzi na upigaji pamoja na uonevu, watu wanafikiri kisasa dunia ya leo sisi bado tunahangaika kudhibitiana, Walay TUMEROGWA na mchawi ashakufwa
 
MAkubwa , madogo yana afadhali , haya yooote ni kujastifai upuuzi na upigaji pamoja na uonevu, watu wanafikiri kisasa dunia ya leo sisi bado tunahangaika kudhibitiana, Walay TUMEROGWA na mchawi ashakufwa
Na kafa kweli kwani ilianzishwa lini mchakato?
 
Serikali imefika sehemu inaanza kutuona wananchi kama hatufai.
Kwa mantiki hiyo sioni kama misingi ya utawala bora inazingatiwa.
 
Back
Top Bottom