jogi
JF-Expert Member
- Sep 25, 2010
- 25,556
- 25,342
Ndege mpya kwishawasili JNIA, zinakuja kwa awamu, mapokezi yalikuwa ya kukata na shoka, "maji kibao" kama vile inazimwa moto, hizo ni mbwembwe na shamra shamra.
Sasa kuna jamaa walikuwa wanaiangalia ile ndege ikitua pale kipawa.
Ghafla naona kuna kijana anajieleza kwa kujiamini sana ikanilazimu nisogee karibu ili maneno yasinipite.
".........zile ndege sio kabisa, we ziangalie kwanza hazina side mirror, zina honi kali kuizidi ya eicher!!!
Halafu pangaboi likiwaka ndege "inavaibreti" kama nokia 3310!!!! Halafu ndege zinatumia ufunguo mmoja, ina maana hazitakuwa zinaruka zote kwa pamoja" eeh si unaona wameileta hii moja wanaupakia funguo ndio wakaiendeleshe na hiyo ya pili wailete!!!
Halafu kosa kubwa kuliko yote ni kuwa hizi ndege ni LHD (left handed drive) wakati sisi huku tunatumia RHD"
Nikaamua kumtolea uvivu
Wewe umepata wapi habari hizo zote!
Kabla hajanijibu akatokea jamaa kanyoa "unga" na kututaka tuondoke pale haraka sana.