Halafu Tanzania ni kama Mungu ametupendelea kwa kutupatia vipaji vya kipekee ktk soka kuliko nchi nyingi Afrika na duniani. Tatizo shetani tuliyeamua kumkaribisha ktk maisha amezuia kabisa tukakosa akili ya kutunza na kuendeleza vipaji.
Huyu kijana Ajibu ni bonge la inside ten la miaka 2 ijayo. Farid Mussa ni winga wa kuchezea ligi kuu angalau ya Ureno ndani ya mwaka mmoja ujao! Ndemla yuko tayari isipokuwa ktk akili yake tu.
Tanzania kuwa na mseto wa wachezaji kama Aishi Manula Ajibu, Farid Mussa, Ndemla, Mwashiuya, Himid Mao, Tshabalala, Mudathir, Kapombe, Msuva, na akina Samaata ktk kipindi kimoja na kwa umri huu ni zaidi ya upendeleo. Tatizo ni nani anawandaa kutoka kucheza mpira wa shule walionao wengi wao sasa hadi kucheza mpira wa matokeo ndani ya miaka 2 ijayo? Nani anawekeza ktk kujenga miili yao, uvumilivu, saikolojia ya ushindi, na njaa ya mafanikio?
Hivi ni zaidi ya vipaji, lakni kwa kuwa sisi tumespecialize ktk saikolojia ya kufeli, itabaki stori