Habari ya usiku huu.
Kijana mwenzenu yamenikuta aisee. Ngoja niingie kwenye mada moja kwa moja.
Kuna binti nilikuwa nae na nilipanga kumuoa,lakini masiku ya hivi karibuni nimeona amebadilika hayuko kama zamani (hapa najua wakubwa wenzangu mmenielewa kwamba kitu kidogo anakasirika na kukuza mambo,nikajua hapa natafutiwa sababu ya kuachwa,machale yakanicheza mapema). Sababu binti namjua vilivyo,nikambana sana akaamua kufunguka hiyo ilikuwa juzi. Akasema ni kweli kuna mtu ameunganishiwa na ndugu zake yaani dada zake na wameanza kuwasiliana na kwa mujibu wake huyo muhusika hakumwambia kama ana mtu na binti amekubali kuolewa na huyo mtu.
Lakini katika kuunganisha doti nahisi huyo muhusika(yaani muoaji) nina mfahamu kabisa. Sasa nimekaa hapa najiuliza je nipotezee nikubali matokeo au nimfate mdau nimwambie ukweli ?
Ushauri wenu tafadhali.