Ndugu zangu,pamoja na ukweli kwamba JK na mafisadi wake watafanya kila jitihada kung'ang'ania madarakani,jambo la faraja ni kwamba USHIRIKA WA WACHAWI HAUDUMU.This time,and perhaps for the first time ever,CCM inakumbana na mgombea makini.Hilo linawapa hofu na tayari kuna dalili za kupanick kwa namna flani.Lakini habari njema zaidi ni possibility ya wao kwa wao kufanyiana ufisadi.Wengi tunakumbuka namna fedha za EPA zilivyoibiwa kwa minajili ya kumsaidia JK lakini mafisadi wakapiga panga la haja.Kilichomsaidia JK ni sapoti ya Mkapa ambaye wakati huo alikuwa rais (hakufanya hivyo kwa mapenzi yake bali shinikizo).Sasa,kwa kipindi hiki JK ana kazi mbili kubwa:moja,kuhakikisha anashinda uchaguzi na kubaki madarakani,na pili,anatengeneza mazingira ya kumnusuru pindi "kura zisipotosha".Wanaweza kuchangishan fedha za kutosha lakini zikaishia mifukoni mwa mafisadi,ambao nao wanahangaishwa na mambo mawili:kuhakikisha JK anabaki madarakini ili azidi kuwalinda na pia wanajijengea mazingira ya "kujinusuru" pindi upepo ukienda vibaya.
Tunaweza kupata ahueni kutoka kwenye mwenendo wa kura za maoni ndani ya CCM ambapo yayumkinika kuhitimisha kuwa ya RUSHWA ya msimu huu ni ya KIHISTORIA.Japo Dkt Slaa ana muda mfupi kujitengenezea mazingira ya ushindi mkubwa,JK naye ana kazi ya ziada ya kutuliza mzuka wa walioangushwa ndani ya CCM...hususan wale waliomwaga mamilioni yao ya kifisadi na kuambulia patupu.Je hatuwezi kubashiri kuwa baada ya CCM kupitisha majina ya wagombea wake kukatokea kizaazaa cha aina yake?
Wakati jukumu kubwa la JK na wapambe wake lingepaswa kuwa ni kumdhibiti Slaa tu,limejitokeza jambo jingine la dharura la kuwadhibiti "wahanga" wa process ya uteuzi wa wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya CCM.Na kwa udhaifu wa JK,hasira za kushindwa za watu kama Malecela,kutanguliza maslahi binafsi kwa mafisadi wenye sauti ndani ya CCM,kuna uwezekano mkubwa wa Dkt Slaa kufanya vizuri kwenye uchaguzi huo.
By the way,lolote linawezekana katika siasa.