Wadhifa wa Mwenezi Taifa CCM ni sawa na DPP, IGP au DCI

Nenda China kamuone mtu anayesimamia Itikadi ya Chama na majukumu yake

Itikadi ndio Injini inayoendesha Chama hivyo kwa sasa Makonda ndiye Dereva wa CCM

Labda nikusaidie, Mwenyekiti anaendesha na Kuongoza Vikao

Katibu ndiye Mtendaji Mkuu wa Chama

Mwenezi ndiye Msimamizi Mkuu wa Ustawi wa Chama

Jumaa kareem 😀
Huyo mwenezi atawadhulumu wengi sana kwa zile itikadi za Chama akikorogea zake!
Hafiki mbali!!
 
Kwa wasomi we hapa sioni jipya hawana tofauti na wasio wasomi ndo wamefikisha nchi hapo alipo, hamna watu bogus kama the so called wasomi wa nchi, huwezi kuamini kwamba profesa Kabudi ni msomi alie bobea, wakina bashiru, hawana impact yoyote kwenye jamii yetu.
Tatizo ni mfumo broo hata umleta Isac Newton hatakuwa na jipya, ukisema ukweli unapotezwa, Ndugai pamoja na ujinga wake lakini 2021 mwishoni alianza kusimama na wananchi system ikampoteza mazima chap
 
Kimsingi umempunguzia madaraka kwa kumfananisha na hao,makonda kwa sasa ni mkubwa kuliko IGP,DCI,DPP na wengine wengine wababaishaji wanaovimba tu kizembe zembe.
IMG_1661.jpg
 
Ndiyo maana nimesema baada ya miaka 10 la saba watakuwa wachache siyo now
Maana yangu ni kuwa kwa mfumo huu wa ccm usitegemee mabadiliko...
Na yakijaribu kutokea hao unaohisi ni wasomi watakuwa brainwashed. Na watafanya ya ovyo kuliko hao STD VII!!

NB: There is an elite capture syndrome operating from the statehouse and ccm corridors
 
Nenda China kamuone mtu anayesimamia Itikadi ya Chama na majukumu yake

Itikadi ndio Injini inayoendesha Chama hivyo kwa sasa Makonda ndiye Dereva wa CCM

Labda nikusaidie, Mwenyekiti anaendesha na Kuongoza Vikao

Katibu ndiye Mtendaji Mkuu wa Chama

Mwenezi ndiye Msimamizi Mkuu wa Ustawi wa Chama

Jumaa kareem [emoji3]
Tofautisha kati ya mwenezi na msemaji wa chama. CCM imesha acha njia kuu ya uendeshaji wa Serikali hasa baada ya vyama vingi. Inajaribu kuturudisha kulekule kwenye chama kushika hatamu enzi za Nyerere, na hii ilikolezwa sana kipindi cha jpm.

Katika hali ya kawaida kama utaratibu ulivyo, Makonda hawezi kukemea mawaziri na maRC. Pamoja na kwamba wote ni wanasiasa lakini ni watendaji wa serikali. Msemaji mkuu wa chama ni katibu mkuu na si mwenezi. Ni kujimwambafai tu na kujivika madaraka hasiyokuwa nayo. Lakini, ukiona swala anaringa nyikani ujue boyfriend wake ni Simba. Inawezekana ameanza kwa mikwara kutegemea mgongo wa aliyemuweka pale.
 
Mim natumia uelewa sio mahaba na twit za sechai. Unapokuwa mwenez swal unaeneza nini? Jibu ilani.
Ilan ndio mpango kaz wa kukuletea maendeleo wewe unaye twiti. Muenez anaeneza ilan
Jukum lako kwenda kusoma ilan kuona barabar za kijijin kwenu vipi zinafikiwa?
Unachanganya kazi za Serikali na kazi za chama wewe. Unataka uturudishe kwenye enzi za wanasiasa kwenda kusimamia madaktari hili hali hawajui hata kuchoma sindano, na kina Mrisho Gambo kwenda kufundisha walimu namna ya kufundisha! Siasa na taaluma ni vitu viwili tofauti. Kazi ya mwenezi ni kuimarisha chama na si kusimamia shughuli za Serikali.
 
Tofautisha kati ya mwenezi na msemaji wa chama. CCM imesha acha njia kuu ya uendeshaji wa Serikali hasa baada ya vyama vingi. Inajaribu kuturudisha kulekule kwenye chama kushika hatamu enzi za Nyerere, na hii ilikolezwa sana kipindi cha jpm.

Katika hali ya kawaida kama utaratibu ulivyo, Makonda hawezi kukemea mawaziri na maRC. Pamoja na kwamba wote ni wanasiasa lakini ni watendaji wa serikali. Msemaji mkuu wa chama ni katibu mkuu na si mwenezi. Ni kujimwambafai tu na kujivika madaraka hasiyokuwa nayo. Lakini, ukiona swala anaringa nyikani ujue boyfriend wake ni Simba. Inawezekana ameanza kwa mikwara kutegemea mgongo wa aliyemuweka pale.
Waziri akitenda Kinyume cha Itikadi atakutana na Rungu la Makonda!
 
Maana yangu ni kuwa kwa mfumo huu wa ccm usitegemee mabadiliko...
Na yakijaribu kutokea hao unaohisi ni wasomi watakuwa brainwashed. Na watafanya ya ovyo kuliko hao STD VII!!

NB: There is an elite capture syndrome operating from the statehouse and ccm corridors
Mkuu watu wana hasira sn now
 
Unachanganya kazi za Serikali na kazi za chama wewe. Unataka uturudishe kwenye enzi za wanasiasa kwenda kusimamia madaktari hili hali hawajui hata kuchoma sindano, na kina Mrisho Gambo kwenda kufundisha walimu namna ya kufundisha! Siasa na taaluma ni vitu viwili tofauti. Kazi ya mwenezi ni kuimarisha chama na si kusimamia shughuli za Serikali.
Right
 
Hapa ni Tanzania 🇹🇿 sio China 🇨🇳
Nenda China kamuone mtu anayesimamia Itikadi ya Chama na majukumu yake

Itikadi ndio Injini inayoendesha Chama hivyo kwa sasa Makonda ndiye Dereva wa CCM

Labda nikusaidie, Mwenyekiti anaendesha na Kuongoza Vikao

Katibu ndiye Mtendaji Mkuu wa Chama

Mwenezi ndiye Msimamizi Mkuu wa Ustawi wa Chama

Jumaa kareem 😀
 
Kwa mujibu wa Katiba yetu iliyojaa mapungufu na mapengo mengi ambayo hao jamaa niliowataja wakiamua kukupeleka mchaka mchaka utajuta kuzaliwa Tanzania.

DPP au DCI wakiamua kukufutia kesi au kukubambikia kesi ya mchongo wanaweza bila shida yoyote chini ya katiba yetu inayoruhusu watawala kuamua chochote.

Nilikuwa sijui Katibu wa Uenezi & Itikadi Taifa ana nguvu kama DCI, DPP. Ahsante Makonda umenifungua macho na kunitoa tongo tongo la ulevi wa madaraka.

Ngongo kwasasa Uturuki.
msalimie sana osman bey na bala hatun
 
Back
Top Bottom