Wadhifa wa Mwenezi Taifa CCM ni sawa na DPP, IGP au DCI

Huyo mwenezi atawadhulumu wengi sana kwa zile itikadi za Chama akikorogea zake!
Hafiki mbali!!
 
Tatizo ni mfumo broo hata umleta Isac Newton hatakuwa na jipya, ukisema ukweli unapotezwa, Ndugai pamoja na ujinga wake lakini 2021 mwishoni alianza kusimama na wananchi system ikampoteza mazima chap
 
Kimsingi umempunguzia madaraka kwa kumfananisha na hao,makonda kwa sasa ni mkubwa kuliko IGP,DCI,DPP na wengine wengine wababaishaji wanaovimba tu kizembe zembe.
 
Ndiyo maana nimesema baada ya miaka 10 la saba watakuwa wachache siyo now
Maana yangu ni kuwa kwa mfumo huu wa ccm usitegemee mabadiliko...
Na yakijaribu kutokea hao unaohisi ni wasomi watakuwa brainwashed. Na watafanya ya ovyo kuliko hao STD VII!!

NB: There is an elite capture syndrome operating from the statehouse and ccm corridors
 
Tofautisha kati ya mwenezi na msemaji wa chama. CCM imesha acha njia kuu ya uendeshaji wa Serikali hasa baada ya vyama vingi. Inajaribu kuturudisha kulekule kwenye chama kushika hatamu enzi za Nyerere, na hii ilikolezwa sana kipindi cha jpm.

Katika hali ya kawaida kama utaratibu ulivyo, Makonda hawezi kukemea mawaziri na maRC. Pamoja na kwamba wote ni wanasiasa lakini ni watendaji wa serikali. Msemaji mkuu wa chama ni katibu mkuu na si mwenezi. Ni kujimwambafai tu na kujivika madaraka hasiyokuwa nayo. Lakini, ukiona swala anaringa nyikani ujue boyfriend wake ni Simba. Inawezekana ameanza kwa mikwara kutegemea mgongo wa aliyemuweka pale.
 
Unachanganya kazi za Serikali na kazi za chama wewe. Unataka uturudishe kwenye enzi za wanasiasa kwenda kusimamia madaktari hili hali hawajui hata kuchoma sindano, na kina Mrisho Gambo kwenda kufundisha walimu namna ya kufundisha! Siasa na taaluma ni vitu viwili tofauti. Kazi ya mwenezi ni kuimarisha chama na si kusimamia shughuli za Serikali.
 
Waziri akitenda Kinyume cha Itikadi atakutana na Rungu la Makonda!
 
Mkuu watu wana hasira sn now
 
Right
 
Hapa ni Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ sio China πŸ‡¨πŸ‡³
 
msalimie sana osman bey na bala hatun
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…