Wadudu na wanyama wakifa huwa wanaenda wapi?

Hata Jeff Epstein alikuwa tajiri lakini mambo aliyokuwa anafanya yalifanya aonekane Hana akili sawasawa. Ndio hata huyo wako nae Hana akili
 
tHi kwakupitia mimi mlaji pale ntakaporudi mavumbini na nikienda peponi naenda nae na nikiwa wa motoni na yeye anakuwa wa motoni kupitia mimi.😀😀
Kwa hili jibu, utakuwa hujala mchana; ebu nenda hapo kwa mama jeni akupe vitumbua vya 300 ule kwanza.
 
Kupitia wewe ndo anakuwa amerudi mavumbini kwahiyo tumbo lako ndo kaburi lake anakuwa anasubiri hukumu tu hapo😎nimeeleweka ee😁
KUmbe hadi kuku wanahukumiwa kwa dhambi😀
Dhambi zao ni kama zetu au wana amri 10 zao za tofauti?😀
 
Kisayansi, wanyama wanapokufa, nishati na miili yao inarudi kwenye mfumo wa ikolojia. Miili yao huoza, inakuwa mbolea, na kurutubisha ardhi ili kusaidia mimea na viumbe vingine kuishi. Hakuna ushahidi wa kisayansi unaoonyesha uwepo wa ufahamu au roho baada ya kifo.


Mitazamo ya Dini za Mashariki (Uhindu na Ubuda)
Katika dini hizi, wanyama, ndege, na wadudu wanaenda kwenye mzunguko wa kuzaliwa upya (Reincarnation au Samsara).

Kitabu cha Isaya na Ufunuo kinataja kuwepo kwa wanyama (kama simba, kondoo, na farasi) katika "Mbingu Mpya na Nchi Mpya." Wataalamu wengi wa Biblia wanaamini kuwa Mungu atawaumba wanyama wapya mbinguni au atafufua viumbe vyake kwa utukufu wake, lakini hakuna adhabu ya jehanamu kwao.

Katika Uislamu, wanyama hawatakuwa na hatima ya kwenda Peponi (Mbinguni) au Motoni (Jehanamu) kama walivyo wanadamu.
 
Jibu la kisayansi limejitosheleza
 
Usiongee sana mkuu ila ukweli ndio huo ukifa umekufa na ndio mwisho wa maisha yako hayo mengine hakuna aliewahi kuthibitisha ni imani tu za watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…