Wadukuzi wadai kuiba taarifa za 74% ya Waisrael wote

Wadukuzi wadai kuiba taarifa za 74% ya Waisrael wote

Sam Gidori

Senior Member
Joined
Sep 7, 2020
Posts
165
Reaction score
417
Wadukuzi wanaojiita Sangkancil wamedai kudukua taarifa binafsi za zaidi ya watu milioni 7 nchini Israel.

Wadukuzi hao wamesema wamedukua taarifa hizo kutoka kwenye tovuti ya CITY4U ambayo hutumiwa na mamlaka za Israel kushughulikia malipo mbalimbali kama bili za kawaida, faini, kodi nk.

Kitengo cha Usalama wa Kimtandao nchini humo kimesema kuwa kinachunguza madai hayo, kikidai kuwa taarifa zilizodukuliwa zinaweza kuwa za muda mrefu uliopita.

Ikiwa madai ya wadukuzi hayo ni ya kweli, hili litakuwa shambulio baya zaidi la mtandaoni kutokea nchini Israel, likihusisha taarifa za zaidi ya 74% ya watu wote nchini humo.

Mdukuzi huyo amesema kuwa anaziuza taarifa alizodukua bila kutaja bei. Taarifa za kudukuliwa kwa tovuti hiyo zilianza kutolewa siku ya Jumapili, huku mdukuzi huyo akionesha baadhi ya taarifa alizodukua ikiwamo vitambulisho vya taifa vya watu, leseni za udereva na bili za kodi kupitia mtandao wa Telegram.

Amedai kuwa ataendelea kutoa taarifa zaidi kuelekea mapumziko ya Mwaka Mpya wa Kiyahudi (Rosh Hashanah).

Hii si mara ya kwanza kwa taasisi za Israel kulengwa na mashambulizi ya kimtandao. Mwaka jana, Wadukuzi wanaojiita Black Shadow walifanikiwa kudukua taarifa za kampuni ya bima na kudai fidia, vinginevyo wangechapisha taarifa hizo katika mtandao wa Intaneti. Kampuni hiyo ilikataa kulipa fidia, na wadukuzi hao wakadai wameuza taarifa katika mtandao wa dark web.

Chanzo: Times of Israel

1631172614208.png
 
Sasa unadukua bills za kazi gani? Si bora angedukua banks akajihamishia hela
Kumbuka kila mtu analipa bills ikiwamo watu muhimu katika idara muhimu za serikali kwa mantiki hiyo kwa taarifa zao za namna hiyo kuwa wazi ina maana kuwa hawako salama
 
kumbuka kila mtu analipa bills ikiwamo watu muhimu katika idara muhimu za serikali kwa mantiki hiyo kwa taarifa zao za namna hiyo kuwa wazi ina maana kuwa hawako salama
Ngoja tuone maana last person kudukua pamoja na kudukua hakulipwa mia. Na hakuna kitu alifanya
 
kumbuka kila mtu analipa bills ikiwamo watu muhimu katika idara muhimu za serikali kwa mantiki hiyo kwa taarifa zao za namna hiyo kuwa wazi ina maana kuwa hawako salama
Pia muambie inaweza kujulikana kuwa katika Government kuna mafisadi, inawezekana bajeti na hizo data zinasoma tofauti kikaanza kunuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taarifa hizo hazina madhara. Wangecheza na taarifa za kibenki na jeshi ingekuwa tishio
 
Back
Top Bottom