Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,319
Miradi ya tovuti (website) si mingi sana hapa nchini ukilinganisha na mataifa yaliyoendelea kiteknolojia. Bado watumiaji wengi wa mtandao hutembelea mitandao ya nje kama vile Facebook, Twitter na Goal.com, idadi ya watumiaji wa mitandao ya ndani sio wengi sana na michache kama Jamiiforums ndio hutembelewa na watu wengi.
Tovuti za mashirika mengi, binafsi na ya Serikali ni kama zimelala kwani ni mara chache kukuta habari mpya humo. Hata baadhi ya mashirika ya habari huwa na tovuti mfu, yaani ambazo hazina maudhui yanayoenda na wakati.
Pamoja na upungufu huu, bado waendelezaje wengi wa tovuti hapa nchini hutumia lugha ya Kiingereza kutengeneza hiziz tovuti. Pamoja na kuandika kwa Kiswahili (tovuti za habari mathalani), bado vitumizi katika tovuti hizi vina maelezo ya Kiingereza. Maneno kama 'home', 'log in', 'register' na kadhalika ni kama haana vibadala vyake kwa Kiswahili.
Tovuti ambazo zimejitahidi walau kuweka muonekano wake kwa Kiswahili ni za nje kama Facebook na Google. Pamoja na jitihada hizi za watu wa nje ya Ukanda wa Maziwa Makuu kutambua umuhimu wa Kiswahili katika mawasiliano ya mtandao bado watumiaji wa Kisahili wamekuwa na mwitiko hasi ka tovuti zenye muonekano wa Kiswahili.
CC: Bisansaba, Canute Temu, FaizaFoxy

Last edited by a moderator: