Waendelezaji wa tovuti wanakiogopa Kiswahili?

Mphamvu

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2011
Posts
10,702
Reaction score
3,319
Miradi ya tovuti (website) si mingi sana hapa nchini ukilinganisha na mataifa yaliyoendelea kiteknolojia. Bado watumiaji wengi wa mtandao hutembelea mitandao ya nje kama vile Facebook, Twitter na Goal.com, idadi ya watumiaji wa mitandao ya ndani sio wengi sana na michache kama Jamiiforums ndio hutembelewa na watu wengi.

Tovuti za mashirika mengi, binafsi na ya Serikali ni kama zimelala kwani ni mara chache kukuta habari mpya humo. Hata baadhi ya mashirika ya habari huwa na tovuti mfu, yaani ambazo hazina maudhui yanayoenda na wakati.

Pamoja na upungufu huu, bado waendelezaje wengi wa tovuti hapa nchini hutumia lugha ya Kiingereza kutengeneza hiziz tovuti. Pamoja na kuandika kwa Kiswahili (tovuti za habari mathalani), bado vitumizi katika tovuti hizi vina maelezo ya Kiingereza. Maneno kama 'home', 'log in', 'register' na kadhalika ni kama haana vibadala vyake kwa Kiswahili.

Tovuti ambazo zimejitahidi walau kuweka muonekano wake kwa Kiswahili ni za nje kama Facebook na Google. Pamoja na jitihada hizi za watu wa nje ya Ukanda wa Maziwa Makuu kutambua umuhimu wa Kiswahili katika mawasiliano ya mtandao bado watumiaji wa Kisahili wamekuwa na mwitiko hasi ka tovuti zenye muonekano wa Kiswahili.

CC: Bisansaba, Canute Temu, FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Hilo linaanzia ktk ufundishaji, Vyuoni hamna kitabu kinachofundisha web-designing kwa Kiswahili.
Labda unitajie maana ya haya maneno kwa Kiswahili ambayo hutumiwa sana, otherwise inabidi developer atafute Kamusi au abuni maneno yake.
1. Share
2. Upload na Download
3. Update
4. Slide-show
5. Widget
 
Mkuu pengine watu hawajajua umuhimu wa lugha katika biashara au hawathamini lugha ya wateja lengwa wao au hawana mwamko na lugha yao? Sio kwamba hakuna visawe vya kiswahili vya kiTEHAMA, vipo ila hawajaamua tu kuvitumia au wanapuuza tu kwa makusudi.
 
Mkuu sio lazima mtu ajifunze kwa kiswahili ndo aweze kutengeneza tovuti kwa kiswahili. Anaweza tumia kiingereza alafu hiyo tovuti "ikijanibishwa" katika lugha inayohusika hata hivyo ni vizuri pia akitumia kamusi. Kuhusu mfano wa maneno uliyotoa visawe vyake katika kiswahili ni kama ifuatavyo:
1. Share - sambaza (katika muktadha wa mitandao ya kijamii)
2. Upload - pakia; download - pakua
3. Update - sasaisha
4. Slide show (nimesahau ila lipo)
5. Widget - Wiji
Nafikiri umepata mwanga mkuu.
 
Hilo linaanzia ktk ufundishaji, Vyuoni hamna kitabu kinachofundisha web-designing kwa Kiswahili.
Labda unitajie maana ya haya maneno kwa Kiswahili ambayo hutumiwa sana, otherwise inabidi developer atafute Kamusi au abuni maneno yake.
1. Share
2. Upload na Download
3. Update
4. Slide-show
5. Widget
Maneno yapo, lakini hayajahamasishwa kutumika ndio maana yanaonekana ya ajabu. Angalia namna watu walivyozoea neno king'amuzi badala ya dikoda wakati neno lenyewe limeanza kutumika juzi.
 
Mkuu pengine watu hawajajua umuhimu wa lugha katika biashara au hawathamini lugha ya wateja lengwa wao au hawana mwamko na lugha yao? Sio kwamba hakuna visawe vya kiswahili vya kiTEHAMA, vipo ila hawajaamua tu kuvitumia au wanapuuza tu kwa makusudi.

Wataalamu wa lugha wakienda redioni wanaishia kufafanua maana za maneno tu, sioni mijadala kama hii ya kukuza lugha yetu.
 
Na wengi wao hawana ufahamu wa TEHAMA, kwa hiyo hawawezi kuongea chochote. Nimeandika makala juu ya Kiswahili katika TEHAMA, RFA waliitumia katika kipindi chao cha redio kinachohusiana na Maswala ya teknolojia. Kumbe tunaweza kuelimisha jamii kupitia mitandao.
 
SAfi sana, nipe kiungo (link)...
 
Wanasiasa wanakejeli hili kila siku.

Pamoja na kukwama kwa wanasiasa, bado wataalamu wetu pia ni wabinafsi na hatujaona juhudi zao za wazi za kushawishi utumiaji wa Kiswahili katika elimu.

Wanaishia kulalamika haya kwenye makongamano na semina zao wenyewe, TUKI hawana hata akaunti ya Facebook ili wawasiiane na watumiaji wengi wa Kiswahili, hawana Afisa wa Mahusiano ya Umma ndio maana harakati zao nyingi zinaishia ndani ya lile jengo kongwe.
 
Miradi ya tovuti (website) si mingi sana hapa nchini ukilinganisha na mataifa yaliyoendelea kiteknolojia. Bado watumiaji wengi wa mtandao hutembelea mitandao ya nje kama vile Facebook, Twitter na Goal.com, idadi ya watumiaji wa mitandao ya ndani sio wengi sana na michache kama Jamiiforums ndio hutembelewa na watu wengi.

Tovuti za mashirika mengi, binafsi na ya Serikali ni kama zimelala kwani ni mara chache kukuta habari mpya humo. Hata baadhi ya mashirika ya habari huwa na tovuti mfu, yaani ambazo hazina maudhui yanayoenda na wakati.

Pamoja na upungufu huu, bado waendelezaje wengi wa tovuti hapa nchini hutumia lugha ya Kiingereza kutengeneza hiziz tovuti. Pamoja na kuandika kwa Kiswahili (tovuti za habari mathalani), bado vitumizi katika tovuti hizi vina maelezo ya Kiingereza. Maneno kama 'home', 'log in', 'register' na kadhalika ni kama haana vibadala vyake kwa Kiswahili.

Tovuti ambazo zimejitahidi walau kuweka muonekano wake kwa Kiswahili ni za nje kama Facebook na Google. Pamoja na jitihada hizi za watu wa nje ya Ukanda wa Maziwa Makuu kutambua umuhimu wa Kiswahili katika mawasiliano ya mtandao bado watumiaji wa Kisahili wamekuwa na mwitiko hasi ka tovuti zenye muonekano wa Kiswahili.

CC: Bisansaba, Canute Temu, FaizaFoxy

mkuu umeongea nondo! na kwa utafiti wangu mdogo tatizo ni lugha inayotumiwa wangetumia lugha inayoeleweka kwa wazawa ingekuwa inatumiwa sana lakini taifa hili tunajifanya kuzungumza kiingereza cha mazoea mfano mis you . love you n.k hivyo ukasumba umetutawala vichwani mwetu sana.
 
Last edited by a moderator:
mkuu umeongea nondo! na kwa utafiti wangu mdogo tatizo ni lugha inayotumiwa wengetumia lugha inayoeleweka kwa wazawa ingekuwa ibatumiwa sana lakini taifa hili tunajifanya kuzungumza kiingereza cha mazoea mfano mis you . love you nk hivyo ukasumba umetutawala vichwani mwetu sana.

Hamasa kutoka kwa wadau ni ndogo, bado hatujajua kuthamini chetu kuanzia lugha, mavazi, hadi bidhaa. Wasomi hawajawa tayari kusapoti harakati hizi wakati wanajua fika kuwa Kiswahili ndio kinaeleweka zaidi...
 
kabisa mkuu cjui lini hawa ndg zangu wataelimika na watapenda vyao .
kwenye mavazi ndo usiseme wanafuata mataifa yaliyoharibika na kushindikana kitabia ambapo cc ndo tungekuwa mfano wa kwanza walau na wao wajifunze na kuiga kwetu japo tu mavazi lakini dah! mimi binafsi naumia sana.
 
Back
Top Bottom