Uchaguzi 2020 Wafahamu baadhi ya Watia nia ya Ubunge wa CCM ambao hawakushinda katika kura za maoni lakini wamepitishwa kugombea katika majimbo yao

Yule mbunge wa Kishapu aliyekamatwa na bunduki 16 naona CCM wamemla kichwa.
 
Shinyanga mjini
matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:

1.Stephen Julius Masele - kura 152

2.Jonathan Manyama Ifunda - kura 65

3.Gasper Kileo - kura 51

4. Patrobas Katambi 12 [emoji736][emoji736]

Hii ndio siasa!!

Sent from my SM-A307FN using JamiiForums mobile app
 
Atimkie upinzani halafu akakae benchi ku-support tu wengine au kuna nafasi ya kugombea?

2010 Bashe naye alifanyiwa hivyohivyo,Seleli mshindi wa pili akaachwa pia akateuliwa Kigwangala ambaye alikuwa underdog.

Hii jeuri hufanyika majimbo ambayo watu huchagua CCM siyo mtu.
 
Hata ningekuwa Mimi, yaani ukatwe kisa uligombama na Ndugai? Hiki ni kigezo Namba ngapi kwenye kanuni za CCM?
ccm wamemuonea masele kisa Ndungai hamtaki awe mbunge aende upinzani mungu atamsimamia
 
Hana jeuri hiyo nakuthibitishia kwa asilimia Mia anakesi mbaya mno tena yenye ushahidi wa kuingiziwa mamilioni ya shilingi kwenye ac yake na aliyekuwa Rais wa Acacia yule anayeozea jela...

..mbona Deo Mwanyika wa acacia alishatoka jela?

..na baada ya hapo alishinda kura za maoni ktk CCM maeneo ya Njombe.

..ukitaka kufukuza waliokula pesa za makampuni ya madini huko CCM utafukuza viongozi wote.

NB:

..hata Waziri wa Nishati Dr.Kalemani aliwahi kuajiriwa na moja ya makampuni makubwa ya madini.

cc T11
 
Tatizo kubwa la bwana mkubwa na Masele lilianzia 2015 mwezi kama huu pale Masele kwa kushirikiana na Mgeja aliyekuwa M/kiti wa CCM kipindi hicho mkoa wa Shinyanga walipoendesha kampeni ya wana CCM kuwataka wasimdhamini JPM...
Kwahiyo huyo mzee alishindwa kumtandika asiteuliwe bunge la Afrika?
 
Hawaelewi hao
 
Kule kilwa kuna jamaa anaitwa ally kasinge alipata kura 12 kama za patrobasi naye kapeta
 
Siyo kwa Shinyanga mjini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…