PSPA Pundit
New Member
- Sep 19, 2013
- 4
- 17
Kuna watu wanaitwa 'ECONOMIC HITMEN". Hawa ni wataalamu wa uchumi wa mataifa ya Ulaya, Uarabuni, na Taifa la Marekani ambao kazi yao Pekee ni kujenga urafiki wa karibu na Marais na watawala wa nchi za Africa na America ya Kusini.
Baada ya kujenga urafiki na ukaribu na Marais pamoja na watawala, Watu hawa hupewa maelekezo na Serikali zao au na Mabilionea wa nchini kwao wenye uhusiano mzuri na serikali zao, kuwashawishi Marais au Watawala kuwauzia Rasilimali za nchi (Kama Bandari na Mbuga za wanyama) kwa Bei itakayowafaidisha wao watawala tu.
Kuingia mikataba ambayo itafaidisha serikali za nje na Mabilionea wa nje Tu, Kuchukua mikopo mikubwa kutoka nchi za nje, mikopo yenye riba kubwa ambayo italifanya taifa kama Tanzania kuwa kwenye utumwa wa kiuchumi kwa miaka mingi. Yule "Peter wa Royal tour" na "Mjomba wa Oman" ni mfano mzuri wa Economic hitmen.
Wale wana kazi moja tu ya kutengeneza ukaribu na mamlaka na kuhakikisha wanaweza kumshawishi kiongozi kuuza rasilimali za nchi au kuzikodisha kwa faida yake na familia yake huku akihakikisha anayekodiwa au kuuziwa atapata faida kubwa sana ya muda mrefu.
Hawa economic hit men huwa wanaifahamu nchi husika vizuri sana, wanafanya utafiti wao kwa ustadi mkubwa sana na wanaandika Ripoti za kweli na kutuma kwa serikali na mabilionea wao. Wanaandika pia ripoti za uongo na zenye lengo la kuwaaminisha watawala wetu kuwa maamuzi yao ya kuuza au kukodisha rasilimali zetu au kuchukua mikopo ya kuumiza taifa ni sahihi.
Hawa Economoc hitmen huwa hawashirikiani na serikali kwa ujumla, wao wanadeal na Rais na watu wake wa karibu tu kama vile viongozi anaowaamini sana au watoto wake, na ndio maana nguvu kubwa na hela nyingi zinatumika (hata kama wananchi wataona hafai) kuhakikisha Rais anaendelea kubaki madarakani ili waendelee kufanya biashara zao huku nchi ikiendelea kuwa kwenye madeni wakati wapambe wanaendelea kutajirika.
Hela za kufanikisha hilo zinatoka nje ya nchi kwa kutumia hiyo mikopo ambayo asilimia kubwa inaishia mfukoni kwa kiongozi husika na wapambe wake, na kwa kuuza na kununua rasilimali za nchi.
Economic hitmen Wanakuwa na urafiki na ukaribu wapambe na familia ya mkuu wa nchi ili wawasaidie kumshawishi mkuu wa nchi afanye wanachotaka kwasababu wanaijua vyema katiba ya nchi kuwa Rais anayo mamlaka makubwa mno kwahiyo na wao wanapita humo humo.
Ndugu Watanganyika nina imani hichi ndicho kinachoendelea kwenye taifa letu.
Tusipopambana kubadili katiba yetu. Marais wataendelea kufaidi rasilimali za nchi yetu huku wakiendelea kuliweka Taifa letu kwenye Madeni yasiyoweza kulipika.