Wafahamu mastaa wa kike Bongo Movie wenye mvuto zaidi

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Licha ya mastaa wengi wa kike wa filamu nchini kubebwa na make up na madawa mbali mbali ya kuongeza mvuto, kuna baadhi ya mastaa wachache ambao wamekuwa waking'ara na kuvutia na mionekano yao ya asili, bila ata ya kutumia make up.

1: LULU MICHAEL
Akiwa katika umri mdogo tu wa miaka ishirini, staa wa filamu bongo, lulu michael, anatajwa kuwa ndiye staa mwenye mvuto zaidi kuliko mastaa wenzie. Achilia mbali make up za gharama anazopaka, lulu anatajwa kuwa na muoenekano mzuri zaidi ata akiwa hajapaka make up, yani ana uzuri wa asili, na ndiye staa anayeongoza kwa kuwindwa na wanaume kila kukicha kutokana na mvuto wake.

2: JOKATE MWIGELO
Mwanamitindo na muigizaji maarufu nchini, jokate mwigelo ,naye anatajwa kuwa staa mwenye mvuto zaidi nchini, licha ya umri wake kusogea, bado staa huyo anazidi kuonekana mrembo zaidi, pia ni mmoja kati ya mastaa wachache wenye mvuto na uzuri wa asili ata bila kutumia vipodozi vya aina yeyote. Dimpozi zake pamoja na tabasamu lake vinatajwa kumfanya staa huyo kuwa na mvuto zaidi kuwashinda mastaa wenzie.

3: ROSE NDAUKA
Namba tatu imechukuliwa na staa wa filamu nchini, rose ndauka. Msanii huyo ambaye hana makuu, anatajwa kuwa na mvuto wa aina yake kuwazidi mastaa wenzie, ata anapokuwa hajapaka kitu usoni, pia uzuri wake umechangia kumfanya apate dili nyingi za filamu apa mjini.

4: ODAMA
Muigizaji wa filamu nchini, jennifer kyaka, ambaye pia ni producer wa filamu naye anatajwa kuwa ni miongoni mwa mastaa wenye mvuto zaidi,ukitaka kuthibitisha uzuri wa mwana mama huyo, jaribu kumtembelea nyumbani kwake hasubuhi wakati akitoka kuamka, unaambiwa staa huyo anavutia zaidi akiwa hajapaka kitu usoni.

5: BATULI
Muigizaji asiye na mkuu nchini,yobnesh yusuph, maarufu kama batuli, naye anatajwa kuwa miongoni mwa mastaa wenye mvuto zaidi bongo ambao hawabebwi na make up, mama huyo wa watoto wawili anawakimbiza mastaa wenzie kwa mvuto, haswa akiwa hana make up usoni

6: HAMISA MOBETO
Mwanamitindo huyu ambaye pia ni muigizaji anayechipukia, nae anatajwa kuwa na mvuto na uzuri wa asili , na inasemekekana uzuri wake wa asili ndio unaompa jeuri mjini, uku ukimpa dili kibao za filamu na matangazo mbali mbali.

7: RIYAMA ALLY
Muigizaji kiwango bongo, riyama ally, naye anatajwa kuwa ni msanii mwenye mvuto zaidi pale anapokuwa hajapaka kitu usoni, mwana mama huyo licha ya umri kumtupa mkono bado anaonekana ni mrembo zaidi usoni na mwenye sura ya baby face.

8 : AUNTY EZEKIEL
Mara nyingi staa huyu anapenda kuwa na muonekano wake halisi, ni nadra sana kumkuta staa huyu kajikwatua, ila unaambiwa anavutia zaidi na ngozi yake ya asili.

9: WEMA SEPETU
Mara nyingi wema sepetu upendelea zaidi kujikwatua na make za gharama, pia inasemekana ni mtumiaji mzuri wa vipodi, ambavyo vinasemekana vinamuaribu ngozi yake, ila unaambiwa bado miss huyo asiyechuja ana mvuto na uzuri wa asili.

10: JACKLINE WOLPER
Achilia mbali staa huyu mwenye mvuto wa aina yake kupendelea kujikwatua mara kwa mara, wanaomjua wanakwambia jack kaumbika kwa uzuri ata ukimkuta kwake akiwa hajajiremba.

Chanzo: GPL
 

Attachments

  • 1433046825877.jpg
    59.6 KB · Views: 2,452
Mi siku nkiwaona live ntatoa maoni make hizi picha za kuedit mmh mtu anajiedit hadi karibia umsahau kama hamisa sijawahi kuona picha yake halisi
 
Mi siku nkiwaona live ntatoa maoni make hizi picha za kuedit mmh mtu anajiedit hadi karibia umsahau kama hamisa sijawahi kuona picha yake halisi

Wanaedit hadi shape?? Au sura tu
 
Beauty is in the eyes of the 'beer-holder'. Sizioni neema za Allah humo shehe!!
 
Aunt Ezekiel ebanae sema ndyo hvyo tena
 
Mimi ninaowaona ni Rose Ndauka na Aunt Ezekel wengine wote kwangu ni chenga tu
 
Mi siku nkiwaona live ntatoa maoni make hizi picha za kuedit mmh mtu anajiedit hadi karibia umsahau kama hamisa sijawahi kuona picha yake halisi

Hamisa mzuri sana ata akiwa hana make up anavutia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…