Zawadini
JF-Expert Member
- Feb 2, 2012
- 2,369
- 1,775
Huenda uko sahihi. Sasa na Wazanzibari kuongozwa na Watanganyika, kwa muktadha huo, sio kuwaonea? mkuu ukiona kwako kwaungua, ujue kwa mwenzio kwateketea.Zanzibar wana wizara yao ya uchukuzi, ujenzi, inayoshughulikia masuala yao ktk sekta hizo.
..sasa kupachika Mzanzibari kuwa ktk wizara hiyo kushughulikia mambo ya Tanganyika naona ni kutuonea.
Wazanzibari wakishika nafasi hizo ni sawa na Watanganyika kwani wote ni Watanzania.ukiacha hilo kuna nafasi kama za Ma-DC ktk wilaya za Tanganyika lakini Wazanzibari wameshika nafasi hizo. Huo pia ni uonevu.
Hili la serikali tatu ni sawa lakini fursa ilikuwepo wakati wa bunge la katiba lakini nyinyi Watanganyika ndo muliozuia hilo. Nadhani bado unayakumbuka ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar wakati ule. Haki ya Mungu kwa uoga wenu hamutafanya lolote na hali itaendelea hivihivi. Tuungane tuondoe hili, siyo kulalamika. Siku nyingine mukiitwa kwenye maandamano mujitokeze.Naamini muungano wa serikali 3 utaepusha dhuluma ambazo Wazanzibari wanazifanya dhidi ya Watanganyika.
Hili unaloliita dhuluma ambazo Wazanzibari mimi silioni. Zaidi naona uchoyo wenu tu na kudhani munaweza kuwatawala Wazanzibari munavyotaka kwa sababu ya mitazamo yao. Hili halitatokea na haki ya Mungu mutaitapika Zanzibar wenyenu bila kushurutishwa.