Eli Cohen
JF-Expert Member
- Jun 19, 2023
- 11,191
- 35,870
Ni Waarabu wenye dini ya kipekee ya Ki-brahamu ambayo hapo awali ilikuwa chipukizi la mbali la Uislamu wa Shia.
Waamini Mungu Mmoja kama walivyo wakristo na Waislam, nabii wao ni Yethro / Yitro, kuhani wa Midiani, baba wa Sipora; Yethro ni baba mkwe wa Musa.
Wafuasi wasiopungua milioni 1 wanaoishi hasa Israel, Lebanon na Syria. Ni Rafiki kwa Wayahudi, Wakristo na Waislamu. Dini yao inaziheshimu sana dini nyingine za Mungu mmoja.
Watu wengi wa Druze wa Syria wanaishi Suwayda, mkoa wa kusini mwa Syria. Hapo ndipo mzozo na ukatili wa hivi majuzi umekuwa ukitokea kwani ISIS na Al Qaeda Sunni (kwa nadharia sehemu ya utawala mpya wa Syria) wamefanya mashambulizi ya kulipiza kisasi na mauaji makubwa, na kusababisha Israel kuingilia kati hadi kushambulia ofisi za mamlaka huko syria.