Wafahamu waarabu/usiyoyajua kuhusu waarabu

The MaskmaN

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2017
Posts
350
Reaction score
764
Habari zenu watu wa JF..

Leo tupate kujua kidogo kuhusiana na hawa watu tunaowaita "Waarabu"...Nimepitia pitia kidogo nchi zao na pia kusoma vitabu vyao vinavyoelezea maisha yao...haya yafuatayo ndio niliopata kuyafahamu kutoka kwa "waarabu":-

1.Neno "uarabu"-"arab" ni neno linalowakilisha asili/tamaduni/culture na sio rangi kama wengi tujuavyo.

2.Duniani kuna nchi 22 za kiarabu,yani waishipo waarabu nazo ni-Lebanon,Syria,Morocco,misri,Tunisia,Iran,iraq,Jordan,kuwait,Qatar,Saudi arabia,Somalia,Djibouti,Comoro,Sudan,Palestina,Mauritania,Algeria,Oman,UAE,Bahrain na Yemen.

3.Waarabu wote sio Waislamu,Na Waislamu wote sio waarabu..ingawa kundi kubwa la waarabu ni waislamu,wachache sana ndio wakristo na Wayahudi.

4.Waarabu ni watu ambao wanawaheshimu sana Wazee na Watawala wao...Ni mwiko sana kukosoa,kudhihaki na hata kumfokea mtu aliyekuzidi umri au aliye mtawala wako.Wana Heshima yenye hofu kubwa yaweza ikawa kuliko taifa zingine zote.

5.Sio Mataifa yote ya kiarabu vazi lao la utamaduni ni kanzu,la hasha,bali yapo mataifa ya kiarabu ni nadra sana kumuona mtu kavaa kanzu nayo ni mojawapo Syria,Misri na Lebanon.

6.Kwenye Lugha ya kiarabu,lugha/ishara ya mwili(body language) ni kitu muhimu sana kuliko hata maongezi yenyewe..Pata muda tizama clips zao.

7.Lugha ya kiarabu ni miongoni mwa lugha inayozungumzwa kwa mfanano karibia mataifa yote ya kiarabu...mfano kwenye kiingereza kuna kiingereza cha wales,australia,marekani n.k

8.Sifa kubwa ya waarabu katika ulaji chakula ni "kutumia mkono" yaani no kijiko no uma..hata awe tajiri kiasi gani dhana yake ya kwanza kwenye kula ni "mkono wake"..Hii imepelekea kupenda kuwa na hotel/migahawa yao mahsusi.

9.Ukiwa kwenye mkutano/meeting ni mwiko kutizama saa iwe ukutani au mkononi,ukifanya hivyo ni ishara ya kuwadharau walioko kwenye mkutano.

10.Mahusiano ya kifamilia/undugu yana nguvu sana kwa waarabu..kwa mfano unaeza kuta nyumba moja wanaishi karibia ukoo/yani bibi wa bibi mpaka babu wa babu na wajukuu wake.

11.Umri hauna nafasi katika kujitegemea yani kuwa huru na makatazo au amri au huduma za wazazi..yani mtu anaweza akafika hata miaka 40 lakini akawa anahudumiwa na wazazi wake.

12.kwa kawaida uchukua zaidi ya mwaka na miezi saba kujua lugha ya kiarabu kwa ufasaha.

13.kinywaji kikubwa katika nchi za waarabu ni kahawa...

AHSANTENI NI HAYO TU YA KWANGU....MENGINE KUHUSU WAARABU NAHISI TUTAYAPATA KUTOKA KWA WACHANGIAJI...[emoji120]
 
Mkuu wewe ulibahatika kupita nchi zipi za waarabu?
 
Wasomali si waarab, never.
 
Ongeza hapo kuwa walipofanya biashara ya utumwa waliwahasi mababu zetu ili wasiweze kuzaliana. Na ndo maana pamoja na kwamba waarabu ndo walikuwa vinara wa biashara ya utumwa na watumwa wengi pia walipelekwa uarabuni hatuwezi kuona masalia ya viazi vya watu weusi kule uarabuni kama ilivyo African-Americans
 
Si kweli.... Mimi babu yangu alipelekwa Mtumwa akaoa muarabu na akamzaa baba yangu, baba alirudi nyumbani na kuoa na kisha kutuzaa sisi. Hata sasa ninavyo type msg hii nipo bara arabu kwa bibi zangu ambao wote ni waarabu.
 
Ushahidi upi uliokuwa nao kuwa mababu zenu wamefanywa watumwa na waarabu? Sijui mnakuwa mnajitoa akili au ndio chuki zenu mkikosa la kusema! 😀 😀 😀 Nyerere aliwaambia wanawake wanafagilishwa barabara unguja kwa maziwa au nani kawafundisha mambo haya? Sio nyinyi mliokuwa mkiwauza ndugu zenu vijijini kwa wazungu kisa unapewa kioo ujitizame?

Nianze kukupangia kila nchi na Colonial Master wake akisha tutajua nani kashamiri kwa biashara ya utumwa?

Mwarabu katoka Oman kaja Zanzibar Enzi hizo, kufika tu, kaifanya Zanzibar Mji mkuu wa Oman. Ivi unaweza kunambia taifa gani limefanya ivo kwa Afrika zaidi ya kuwadharau tu? Nyie na CCM ya Zanzibar mkieneza chuki dhidi ya Waarabu, lakini walivokuja na meli yao kina Balozi wakafunga bandari hamna kazi kuwapisha waarabu waingie, mnajifanya watumwa kabla ya kutumwa 😀
 
Ongeza hapo kuwa walipofanya biashara ya utumwa waliwahasi mababu zetu ili wasiweze kuzaliana. Na ndo maana pamoja na kwamba waarabu ndo walikuwa vinara wa biashara ya utumwa na watumwa wengi pia walipelekwa uarabuni hatuwezi kuona masalia ya viazi vya watu weusi kule uarabuni kama ilivyo African-Americans
Kweli lakini
 
Si kweli.... Mimi babu yangu alipelekwa Mtumwa akaoa muarabu na akamzaa baba yangu, baba alirudi nyumbani na kuoa na kisha kutuzaa sisi. Hata sasa ninavyo type msg hii nipo bara arabu kwa bibi zangu ambao wote ni waarabu.
Tuta amini vipi ndugu
 
Back
Top Bottom