Wafahamu wachezaji kumi bora kuwahi kutokea Tanzania mpaka sasa

Vipi Chuma (Beki Na.3 wa Mtwara) aliyekataa kuhamia Dar kujiunga na Simba au Yanga mpaka alipostaafu mpira? Vipi Kitwana Manara aliyechezea Taifa kama golikipa na kama mshambuliaji Na 9? Vipi Sembuli wa Morogoro aliyekuwa na shuti kali sana kwenye penati au free kick? Vipi Kibaden wa Simba aliyepewa hadhi ya ufalme huko Songea mpaka miaka ya 70/80 kukawepo msemo kwamba Tanzania kuna King mmoja tu na Lord mmoja: King Kibaden na Lord Rajpar (aliyehusiana na scandal ya meli ya Tanzania)?
 
Mkuu una kumbukumbu nzuri. Bila kumsahau Maulid Dilunga.
 
Mkuu hawa magwiji niliwasahau, nimeipandisha pale juu ili tufike kwenye 70 badala ya 50.
 
Kuna fundi alikuwa anaitwa Hamis Thobias "Gagarino"

Kwenye hiyo listi ni aibu kumkosa Charles Boniface Mkwassa

Hussein Masha atakosaje kwenye top 50

Marehemu Gibson Sembuli

Dua Said

Razak Yusuf " Careca"

Nteze John

Malota Soma

Method Mogella "Fundi"
 
Kwa ukongwe wangu sina neno kabisa na list yako hasa baada ya kumuona edibily mnyama na mwamba kizita.
 
Mkwasa na Sembuli niliwasahau ila nimewapandisha pale juu.. wengine nimewataja tayari na kuna mdau kawataja nikaipandisha post yake.
 
Sijui umetumia vigezo gani, ila Mrisho ngasa ni zaidi ya msuva....wote tumeonaa ila hao wazee sijui me nimeanza kua na akili ya kufatilia hao watu kuanzia 2005...
Mnawapamba tu wa zamani
 
Kuna Method Mogela, Abeid Mziba, Zimbwe, Issa Athumani, Keneth Mkapa, Thomas Kipese,Salvatory Edward...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ