Wafahamu Wafadhili Wakubwa Wa Mashirika ya Hisani Na Sifa Zao (Major Gift Donors and Their Traits)

Joined
Feb 5, 2022
Posts
38
Reaction score
60
1732361821148.png

Wafadhili wakubwa yaani “Major Gift Donors” ni watu ambao wanatoa kiasi kikubwa cha ufadhili kwa shirika, ili kuliwezesha shirika kutekeleza programu na miradi yake kikamilifu. Tafsiri ya mfadhili mkubwa inatofautiana kutoka shirika moja na jingine, kimsingi hakuna kiwango maalum kinachoonyesha kwamba huu ni ufadhili mkubwa na huu ni ufadhili mdogo. Kwa mfano; shilingi 100,000 kwa mwaka/miezi kadhaa kwa shirika moja inaweza ikawa ni kiwango kikubwa cha ufadhili na vile vile shilingi 50,000 kwa mwaka/miezi kadhaa ikawa ni kiwango kikubwa cha ufadhili kwa shirika lingine.

Wafadhili wakubwa ndio msingi na mustakabali wa shirika, kwa sababu wanachangia kiasi kikubwa cha ruzuku kwa shirika. Hivyo ni jukumu la uongozi wa shirika kuwa na utaratibu wa kuwatafuta wafadhili hawa. Mchakato wa kutafuta wafadhili wakubwa (Major Gift Donors) una sifa zifuatazo;
  • Unachukua muda mrefu, kuanzia; mwezi, miezi mpaka mwaka wakati mwingine ili mfadhili akubali kulifadhili shirika.
  • Unahusisha mawasiliano ya ana kwa ana (face-to-face solicitation) ambayo yataongozwa na mtu kutoka kwenye shirika anaejuana na mfadhili tarajiwa (prospect)
  • Ufadhili unaweza kutolewa punde baada ya mfadhili kukubali au baada ya muda kupita (pledged over time)
  • Ufadhili unaweza kutolewa kwa mfumo wa fedha, wakfu au urithi (planned gifts)
Wafadhili wakubwa wamegawanyika katika makundi tofauti tofauti, miongoni mwa makundi hayo ni kama ifuatavyo;
  • The Devout: Kundi hili linabeba asilimia 21 ya wafadhili wakubwa. Hawa ni wafadhili ambao wanasukumwa na sababu za kidini kwenye ufadhili wao, hivyo mara nyingi ufadhili wao unatolewa kwa taasisi za kidini kama vile misikiti, makanisa, shule za kidini, hospitali za kidini n.k.
  • The Investor: Kundi hili linabeba asilimia 15 ya wafadhili wakubwa. Hawa wanafadhili mashirika kwa lengo la kupata punguzo la kodi. Hii hutokea kwenye nchi ambazo mifumo yake ya kodi ni rafiki kwa shughuli za hisani kama nchi ya Marekani.
  • The Socialite: Kundi hili linabeba asilimia 11 ya wafadhili wakubwa . Hawa ni wanachama wa mitandao/makundi ya kijamii (social networks) ambao wanaamini kusaidia shirika la kijamii ni jukumu la kijamii, na wao kwa sababu ni wanajamii, basi wanapaswa kufanya hivyo.
  • The Altruist: Kundi hili linabeba asilimia 9 ya wafadhili wakubwa. Hawa wanasukumwa na ubinadamu pia na moyo wa kutoa pindi matatizo yanapotokea kwenye jamii. Mara nyingi wafadhili wa namna hii pindi wanapofadhili, hawapendi majina yao kujulikana.
  • The Repayer: Kundi hili linabeba asilimia 10 ya wafadhili wakubwa. Hawa ni wafadhili ambao kwa kipindi fulani huko nyuma walifaidika na huduma za shirika, hivyo wanafadhili ili kurudisha fadhila kwa shirika husika. Mfano wa kundi hili ni wagonjwa waliowahi kutibiwa na hospital fulani na kupona maradhi yao au ndugu wa wagonjwa ambao kitaalamu tunawaita “grateful patients and families of grateful patients”, wahitimu wa chuo fulani “alumni and alumnae” n.k.
  • The Communitarian: Kundi hili linabeba asilimia kubwa zaidi ambayo ni 26. Kundi hili linaamini kwamba ufadhili kwa mashirika ya hisani ni muhimu na unahitajika ili kuboresha maisha ya jamii.
  • The Dynast: Kundi hili linabeba asilimia 8 ya wafadhili wakubwa. Hawa ni watu ambao wanatoka kwenye familia zenye utamaduni wa kutoa kwa ajili ya matatizo ya kujamii na zinaamini kwenye utoaji.
Kwa kuhitimisha, mashirika ya kajamii zikiwemo hospitali, shule, vyuo, makanisa , misikiti, asasi za kiraia, vituo vya utamaduni n.k hayana budi kufahamu sifa za kundi hili la wafadhili ili yaweze kuandaa programu maalum za kuwaingiza kwenye utaratibu wa uchangiaji wa shirika (Major Gift Donor Cultivation Program). Hii ni kwa sababu; kikanuni ni asilimia 20 tu ya wafadhili (ambao ni “major gift donors”) wanahudumia asimilia 80 ya mahitaji ya ufadhili kwa shirika.
Mchakato wa kumtafuta na kumuingiza mfadhili kwenye utaratibu wa uchangiaji kwa Shirika unapaswa kuendeshwa kwa umakini mkubwa na uvumilivu. Asilimia 85-90 ya muda wa mchakato inapaswa kutumika kwenye utafiti, ukusanyaji wa taarifa za mfadhili husika na vikao, wakati aslimia 10 au 15 tu ya muda wa mchakato ndio itatumika kuomba ufadhili (asking for money)​

Article By;

OMAR MSONGA
CONSULTANT
Project Management, Strategy, Fundraising & Training
For Consultation Service; Call: +255 719 518 367
Email: msongatheconsultant@gmail.com
DAR ES SALAAM
TANZANIA
 
View attachment 3159587

Hivi wafadhili wanapata wapi faida? Kwa mfano shirika la MDH linafadhiliwa na pepfar na CDC je pepfar na CDC wanapata wapi faida?
 
Back
Top Bottom