Wafahamu wanawake wa shoka Bongo Movie

Wafahamu wanawake wa shoka Bongo Movie

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Achilia mbali ongezeko la wingi wa waigizaji wa kike ndani ya bongo movie, ni wanawake wachache tu wenye kutambua thamani ya utu wao na hata kazi ya uigizaji walioamua kuifanya. Waliamua kuweka kila kitu pembeni na kuamua kuitumikia sanaa kwa mapenzi yao yote na nguvu zao zote. Heshima ziwaendee kwao.

1. MONALISA
Ni mwanamama muigizaji ambaye heshima yake haijawahi kushuka toka aanze kuingia kwenye tasnia hiyo, ni kati ya waigizaji makini na wanaolewa nini anatakiwa kufanya akiwa location, japokuwa amekuwa nadra kuonekana kwenye filamu za kibongo, hilo halijamfanya ashuke kiwango sokoni ata kwenye uigizaji, bado ni dhahabu kwenye kiwanda cha filamu apa Bongo.

2.JOHARI
Safari yake ilianzia kaole , enzi hizo wakiigiza kwenye michezo ya Tv, alisota sana kabla ya kuibuka kinara wa movie za kibongo, nadhani ndiye msanii wa kike aliyewa inspire wadada wengi kuingia kwenye uigizaji. Kama ulikuwa unadhani sasa ivi kafulia basi umekosea, sasa ivi yupo nyuma ya camera akipiga mzigo kama kawa ndani ya kampuni yake ya RJ company, pia ni producer wa film ndani ya kampuni hiyo, anavuta mkwanja kama kawa kupitia kampuni yake na ray.

3. ODAMA
Alikula msoto wa nguvu kabla ya kumiliki kampuni yake ya filamu iitwayo Jfilm 4life. Ni kati ya wanawake wachache ndani ya bongo movie wanaofanya vizuri sana , pia kazi zake zinafanya vizuri sana sokoni, anaendesha maisha yake kupitia fani ya uigizaji.

4.LUCY KOMBA
Unaikumbuka movie ya UTATA iliyowahi kutikisa miaka ya nyuma?, huyu bidada alihusika sana ndani ya movie hiyo, kwa taarifa yako tu kama hujui, bila huyu akina Irene uwoya na yusuph mlela pamoja na wolper wasingeleta mbwe mbwe zote apa mjini , alichangia sana kuwafikisha apo walipo
japokuwa wengi hawamfahamu

5.WASTARA
Ningependa kumwita SUPER WOMAN, achilia mbali ajali mbaya ya gari iliyosababisha kupoteza mguu wake mmoja, bado hakuacha kuitumikia kazi ya ugizaji tena mara kumi zadi ya ilivyokuwa mwanzo, kupitia kampuni yao ya wajey wametengeneza filamu Kali kibao ikiwemo ile ya VITA iliyowachanganya watanzania wengi na kuwaacha midomo wazi, huyu mama ni moto wa kuotea kazini.anaendesha maisha yake kupitia sanaa.

6.NISHA
Kwa wafuatiliaji wa bongo movie, kipaji cha huyu Dada hakiitaji kumulika na tochi, ameonyesha juhudi Kali sana ndani ya kampuni ya ya nishas film production, ni kati ya wasanii wachache wenye moyo wa kujituma wawapo kazini, pia anaelewa sana nini anatakiwa kufanya awapo kazini.

7.RIYAMA ALLY
Unaikumbuka movie Kali ya FUNGU LA KUKOSA ? Unaikumbuka filamu ya MWASU? Rudi kwenye KIGODORO halafu itafakari filamu ya BEST WIFE bado ujaelewa tu namaanisha nini? Kaangalie tena MY DARLING , Huyo ndiye riyama sihitaji nguvu zaidi kumuelezea. Wengi mnajua habari yake.

8.DOKII
Binafsi ningekuwa na uwezo wa kum manage huyu msanii, ningefanya hivyo , huyu ni dhahabu iliyojificha, ana kipaji hatari sana , inaitaji uwe na jicho la tatu kuliona hili, alifanya miujiza sana kwenye film ya SCANDAL , waliyoiona hii watasimulia. Hakuna mwanamke aliyewahi kunishangaza bongo movie kama yeye, yupo poa sana japokuwa ana mapepe flani.

9.MAINDA
Huyu kwangu ni mwanamke wa shoka , anajiamini sana awapo mzigoni, hakawahi shuka kiwango toka miaka hiyo, muangalie kwenye HEKIMA.

10. CATHY RUPIA
huyu naomba nisimuelezee.
 
Kiukweli kuna wasanii wakike wanajiheshimu....ingawa wana mapungufu yao ila naona wanajitahidi kukaa mbali na skendo chafu....hongera zao
 
Binamu hao wengine ni mastaa wa IG na Shigongo tu ila nisiseme sana kwa vile sikuiz siangalii hizo movie kama huyo Nisha nimemuona marachache ila may be yuko vizuri ila kumbuka wako wengine japo wana muvi chache wanajua wanacho kifanya sio kuuza sura tu mf. Monalisa, Thea, Riyama, Kemmy ingawa sikuiz haigizi hizi top 4 zangu hawa black beuties wakipewa kazi hawafanyii mzaha wana vaa uhusika kamili.
 
Ni bahati mbaya sana msanii Dokii (Umy Wenceslaus) hatambui kipaji chake cha uigizaji.Kama vile hana mshauri mzuri. Mara eti anataka kuwa mwimbaji, mara eti kaokoka, mara yupo kwenye misafara ya wanasiasa nk. Angetulia na kipaji chake cha uigizaji wa lafudhi ya Kiswahili cha Kenya, angekuwa mbali sana.Lafudhi yake ya kikenya ingetosha kabisa kuanzisha kipindi cha uchekeshaji kwenye tv zetu hapa nchini. Amka sasa Dokii, achana na wanasiasa vigeugeu!
 
hawa wanotusumbua hapa nazani ni wadau wa lile jukwa la siasa
wao kila mda wanawaza dis tu!
warumi watu wa namna hii wasikuumize kichwa , tena nazani wao ndo wamekosa kazi ya kufanya maana hatuoni hoja ya maana waliyotuletea ndani ya jukwaa husika zaidi ya kuonesha chuki zao za kishoga

Ahsante mkuu
 
Last edited by a moderator:
Achilia mbali ongezeko la wingi wa waigizaji wa kike ndani ya bongo movie, ni wanawake wachache tu wenye kutambua thamani ya utu wao na hata kazi ya uigizaji

wapi Kemmy, Coletha, Thea? hawa nao ni iron ladies kwenye sanaa ya filamu.
 
Wapi Jenifa Kyaka aka Odama.?
 
Hee binamu ushabadili jina na kujiita Soud brown.

Binamu kuna mtu alinivuruga nikampa mvua ya cheche hatimaye ban ila soon ntarud na my real name warumi hili la Gossipcopwarumi kwa mda tu na itakuwa account yangu ya ziada endapo yatatokea maafa kama haya , usiogope swaga zile zile, radha ile ile sema nimeongeza utamu zaidi ili nizid kuwachanganya haters
 
Last edited by a moderator:
yeah,wapo vzur sana hao wadada!!!! wanaonyesha kwel wanawake wanaweza big up kwao
 
Kuna mdada anaitwa Mariam Ismail,nampenda sana....Batuli nae yuko vizuri ila al in al Irene Paul,no one can touch her shoes

Kacheza movie kama Love and Power ya Kanumba,The Shell ya Ray,Kibajaji akiwa na Mboto n.k
 
Binamu kuna mtu alinivuruga nikampa mvua ya cheche hatimaye ban ila soon ntarud na my real name warumi hili la Gossipcopwarumi kwa mda tu na itakuwa account yangu ya ziada endapo yatatokea maafa kama haya , usiogope swaga zile zile, radha ile ile sema nimeongeza utamu zaidi ili nizid kuwachanganya haters

Hahaaa pole sana binamu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom